Friday, June 18, 2010
Scientific research and society - a lecture by Kofi Annan
Venue: Swiss Federal Institute of Technology (ETH) - Zurich, Switzerland
Today I was fortunate enough to attend an overbooked lecture by Mr. Kofi Annan, the former UN-SG and Nobel Peace Prize Laureate. For this year's Richard R. Ernst Lecture at the ETH Zurich, Mr. Annan delivered a captivating lecture on the role of scientific research in solving the needs of society . He urged young researchers to delve into research that crosses boundaries of their fields through interdisciplinary work and international collaborations with less technological advanced nations. Addressing a multitude of young researchers and students, Mr. Annan pointed out that scientists should provide the necessary leadership in research policy when political support is lacking. This could be through creating innovative solutions to societal needs that gain public support of the target communties. He pressed on the need of academics to refuse to remain in the ivory-tower, but rather become actors through research that makes a lasting impact to society. During the lecture, he quoted the Indian statesman and foremost actor in its R&D revolution, Jawaharlal Nehru, who once said "we are too poor to not invest in science and technology", to highlight the importance of science and technology for solving incessant problems of the south - food shortage, climate change and diseases of poverty.
The full lecture
(c) ETH Zurich, ITS-MMS
Below are amateur video clips of the panel discussion with Kofi Annan chaired by the 1991 Chemistry Nobel Laureate Prof. Richard R. Ernst.
Thursday, June 17, 2010
Does the world need nuclear energy?
Wednesday, June 16, 2010
Tuesday, June 15, 2010
A family tree for humanity
Monday, June 7, 2010
UNAWE-Tanzania
Mara nyingi nikitembelea tovuti ya UNAWE-Tanzania, nashindwa kujizuia kujiuliza maswali mengi. Ingekuwa vipi kama ningefundishwa na timu ya kaka Mponda? Je, kama ningeoneshwa mwezi, sayari nyingine, nyota na vimondo wakati bado niko mdogo, mambo yangekuwa tofauti? Kusema ukweli kuna wakati nawaonea donge watoto wanaopewa nafasi na UNAWE-Tanzania. Na nina uhakika juhudi zao zitazaa matunda ambayo yataleta mabadiliko kwenye jamii yetu kwa namna moja au nyingine.Nakumbuka nilikuwa napenda sana masomo ya sayansi. Na nilijifunza jinsi ya kukokotoa maswali ya lenzi (i.e. ray optics), nilikariri majina ya sayari zote (na idadi ya miezi yao) na hata umbali wao kutoka kwenye jua. Lakini nilikuja kuiona telescope kwa mara ya kwanza nilipokuwa kidato cha pili! Nadhani unaelewa kwanini nawaonea donge wadogo zangu.
Wiki chache zilizopita, UNAWE-Tanzania walipokea vitabu, CDs na vifaa vingine muhimu vya kufundishia. Bahati mbaya au nzuri, kuna baadhi ya vitabu ambavyo itakuwa vema vikitafsiriwa kwenye lugha ya Kiswahili. Kwahiyo, wasiliana nao kama unaweza kuwasadia.
Nakusihi utembelee tovuti yao mara kwa mara ili kufuatilia vitu wanavyofanya. Kama hutaweza kuwasaidia kwenye mradi huu wa kutafsiri vitabu, nina uhakika hapo baadae unaweza ukawasaidia kwa njia nyingine.
Pongezi zangu ziwaendee UNAWE-Tanzania! Nitaendelea kuwatupia jicho kama kawaida yangu.
Tuesday, June 1, 2010
Waafrika tuna asili moja?
Kwa muda mrefu nimekuwa nikiumia roho mno kwa jinsi watu kutoka Afrika tunavyolundikwa kwenye kundi moja kiasilia. Kukiwa na tatizo utasikia, waache hao, ni tabia ya Waafrika hio, hawatakoma. Bara/nchi yao imelaaniwa.
Ukweli ni kwamba bara letu lina watu wenye asili na tofauti nyingi mno kimaumbile, kiutamaduni na hata ukiingia kwenye chembe chembe za DNA. Ukiangalia bara la Ulaya, Wajerumani wamepakana na Wafaransa, lakini watu hawa hawapendi kabisa kufananishwa. Ukienda Amerika ya Kusini, ni mwiko kumuita mtu anayetoka Colombia Mbrazili.
Utafiti unaonesha kwamba idadi kubwa ya watu wenye asili ya Afrika wana maumbile mengi na tofauti kuliko watu katika mabara mengine -- hasa ukiangalia chembe chembe L1, L2 na L3 mtDNA (Krings et al, 1999).
Wanahistoria waliojaribu kutafuta jinsi ya kuelezea asili ya Mwafrika, walifanikiwa kusambaza mawazo yao pande zote za dunia. Mengi ya mawazo hayo yawezekana yalikuwa ya kudhani tu au imani. Inasemekana kuwa asili ya Mbantu ni misitu ya Kongo. Ingawa yawezekana ikawa ni kweli, nina hofu ikawa ni imani ya wenyeji wa pale waliodhani kuwa wako katikati ya dunia. Na mtafiti aliyefika pale hakuweza kupata mawazo ya staarabu, makundi au falme nyingine zilizokuwa mbali na eneo utafiti huo ulipofanyika.
Kwahiyo elimu iliyopatikana hapo haikuwa ya kutosha au tuseme ilikuwa hafifu. Ingawa mtafiti huyo alilifahamu hilo, aliamua kufanya hitimisho kuwa Wabantu wote walitokea eneo lile. Ninaweza nikahisi kuwa, Kibantu asili kama ilivyokuwa Kilatini na sasa Kiingereza, ilikuwa lugha ya wasomi wa kale hapa Afrika. Sasa, idadi ya watu wenye asili tofauti ilivyokuwa inaongezeka, lugha nayo ilikua na kubadilika taratibu ingawa iliendelea kuwa na asili yake miaka nenda rudi. Hitimisho hili halina uhakiki kuwa asili ya Wabantu na hasa watu wa kusini mwa jangwa la Sahara wawe na asili ya misitu ya Kongo. Cha kushangaza, chembe L0 mtDNA inayosemekana kuwa mzazi wa L1, L2 na L3 mtDNA, inahisiwa kuwa na chanzo chake Afrika Mashariki.
Kwanini Waafrika tukubali kuwekwa kwenye kundi moja kiasilia? Je, uanzishwaji wa Umoja wa Afrika unaangalia tofauti kubwa zilizopo za utamaduni na asili kati ya makundi mbalimbali hapa Afrika kwa nia ya kuboresha sera za muungano huo? Makala hii itaendelea na uchambuzi wa kina zaidi kuhusu hili jambo.
Picha/ramani inapatikana hapa.
Monday, May 24, 2010
Watanzania Tunaogopa Sayansi? Sehemu ya Pili
Particles. Mlipuko. Mlundiko wa data. Haya ndio yatokanayo kwenye matembezi niliyofanya na wenzangu kwenye saiti ya tafiti ghali kuliko zote duniani: saiti ya Large Hadron Collider pale CERN. Ndani ya bomba la duara lenye uzingo wa kilomita 30 hivi, protoni zinakimbizwa kwa spidi ya kilomita 299000 kwa sekunde ili kusababisha mlipuko mdogo pindi zinapogongana. Mlipuko huu unatumiwa kufahamu sifa za vihimili viundavyo maada (matter), pamoja na siri mbalimbali kuhusu ulimwengu wetu.

Bajeti ya utafiti wa CERN ni T.Shs Trilioni 1 kila mwaka. Wengi wetu tunaweza kushikwa na hisia na kuwakasirikia na kuuliza kwanini wanatumia pesa nyingi hivi kwa tafiti kama hizi zisizokuwa na uhakika? Wakati huohuo mamilioni ya watu wanakufa kwa ukimwi, malaria na njaa kila mwaka. Binafsi ninadhani mpaka tutakapofahamu umuhimu wa sayansi kwa manufaa yetu wenyewe (waTanzania), hatuna haki ya kuwa na hisia hizi. Sayansi yetu ya kupambana na haya majanga inahimizwaje? Au jamii yetu tutabaki kushabikia akina dokta manyau tu.
Spidi ya hatua zilizopigwa na wenzetu kwenye sayansi inastaajabisha. Na kutambaa kwetu katika lengo hili hili halitazaa matunda kama hatutaamka. Tunahitaji kufinywa na kuhimiza sayansi nyumbani.
Monday, May 3, 2010
The next Einstein
Mchakato wa kuanzisha kijiji hiki aliuanza mwaka 1987, na hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini mpango ulipewa heko na jamii nzima ya wanazuoni na hata hayati Mwl. Nyerere 'aliupigia debe'. Ofisi za IVST zilizinduliwa pale AICC Arusha, na mpango ulikuwa kijiji hiki kianzishwe Arusha. Cha kusikitisha mamlaka ya Ardhi ilitupilia mbali ombi la kibali cha kiwanja, kwa sababu mbalimbali ambazo hadi leo hii hazifahamiki. Na huu ndio ulikuwa mwanzo wa mwisho wa ndoto ya Prof. Shayo kuanzisha kijiji hiki muhimu.
Katika muongo huu, ndoto ya Prof. Shayo yaweza kutimia. Kuna mpango mkubwa wa kuanzisha vituo vya sayansi kama vya Prof. Shayo barani Afrika unaosimamiwa na mwanafizikia maarufu kutoka bondeni Prof. Neil Turok. Kupitia chuo alichokianzisha cha African Institute for Mathematical Science chenye makao makuu huko bondeni, Prof. Turok nae ana ndoto ya kujenga vituo kama hivi kila kona ya bara la Afrika ili kusaidia kukuza mafunzo ya hisabati na sayansi. Ndoto yake ni kumpata gwiji wa fizikia/hisabati kutoka Afrika atakayeleta mabadiliko katika sayansi kama aliyoleta Albert Einstein katika karne ya 20. Tanzania ni moja ya nchi ambayo kituo cha AIMS kinatarajiwa kujengwa. Hadi hivi sasa mchakato huu bado upo katika majadiliano.
Tunajua kuwa elimu ya sayansi na hisabati inazembewa na wengi nchini. Ila hii isiwe sababu ya kutohimiza suala hili kwa hali na mali kwa wanafunzi wetu. Nina imani pia, Tanzania yaweza zalisha akina Einstein iwapo tukiwa na jitihada maalumu kusimamia somo la hisabati katika mitaala ya elimu yetu. Kwa wanaosimamia mazungumzo ya mchakato wa kuanzisha kituo cha AIMS Tanzania, msituangushe.
Sunday, May 2, 2010
Motisha
Je, umeshawahi kufikiria kwa kina kuhusu suala la motisha? Nini hukusukuma kufanya shughuli zako za kila siku? Umeshawahi kujiuliza kwanini unaenda shule au kazini? Nina uhakika kuwa baadhi yenu mtaanza kufikiria watu ambao wanateseka ili tu mkono uende kinywani. Lakini hapa nazungumzia wale ambao kwenye jamii zetu huonekana kufika kwenye kilele cha mafanikio; wanaonekana kama wana kitu zaidi. Ni kipi hicho basi? Tunaweza kujifunza au kuwafundisha wadogo/watoto zetu? Au ni kitu ambacho mtu anazaliwa nacho -- na mazingira na mazingara hayawezi kukibadilisha?
Nimepata nafasi ya kujadili hili na marafiki zangu wengi, lakini mpaka sasa hivi sijapata jibu ambalo limeniridhisha. Labda maisha pamoja na lengo la maisha yetu hayawezwi kuelezwa kwa maneno.
Nina uhakika taswira za watu mbalimbali ambao unajua wanafanya kazi zao vizuri zinaanza kutokea kwenye fikra zako. Pia, unajua hadithi zao jinsi walivyofanikiwa kwenye shughuli zao.
Kuna wale ambao hadithi zao hutupa motisha; hulka zao tu hutosha kutusaidia kutupa msukumo kwenye maisha yetu kwa namba moja au nyingine, hasa pale motisha zetu zinapopungua kutokana na vikwazo vya hapa na pale. Mimi binafsi nina orodha ndefu kiasi (mama yangu akiwa namba moja!), lakini mara nyingi napenda kujikumbushia 'safari' ya William Kamkwamba:
Hakuridhika na kuishia hapo. Angalia alivyorudi miaka miwili baadae:
William, I salute you. You are one of my heroes!
Saturday, April 24, 2010
Viumbe hai nje ya sayari yetu
Je, kuna wakati unakaa chini na kutafakari mwanzo wako ulikuwaje? Nini kilikuwa kinatokea kwenye maisha yako kabla hujaanza kuota meno?

Au kama una bahati, ulikuwa na watu ambao walikuwa wako tayari kukuelezea mambo mbalimbali yaliyokuwa yanakutatiza. Na kama ulikuwa una bahati sana, ulizungukwa na watu ambao walikuwa wako tayari kukupa hata vifaa vilivyokusaidia kuona na kuelewa vitu gani hasa vipo karibu na sayari yetu.

Ruka karne 4...
Kizazi chetu kimekuwa na bahati ya kushuhudia mapinduzi katika teknolojia ambayo hutusaidia kujifunza mambo mbalimbali na kuturahisishia maisha kwa ujumla. Bahati mbaya teknolojia hiyo hiyo imekuwa inatuletea zahma mara nyingine (soma kuhusu Manhattan Project 1942-46; huu ni mjadala wa siku nyingine)!
Ukitafakari kwa makini utaona kuwa tabia za watoto wadogo na sayari yetu zinarandana. Wakati uko mdogo unakuwa kwenye fikra zako ambazo hakuna kiumbe mwingine anazielewa na unadhani uko peke yako. Lakini kadri unavyozidi kukua ule mtazamo unabadilika -- watu walio karibu nawe hukusaidia kuelewa yanayokuzunguka.
Kwa upande mwingine, sayari yetu tulidhani ni pekee. Lakini sasa hivi tunajua kuwa kuna vitu vingine ukiacha hii dunia. Teknolojia (ambayo unaweza kuilinganisha na watu wanaomzunguka mtoto mdogo) imetusaidia kujifunza nini hasa kilichopo karibu na hii sayari yetu.
Kuna wanasayansi ambao wanajaribu kutafuta viumbe hai nje ya sayari yetu. Na hawaishii hapo tu; wanaamini wameanza kuona dalili za uwepo wa viumbe vyenye akili. Hapa nazungumzia intelligence -- uwezo wa kufikiria, kutatua matatizo, kuwasiliana, kujifunza vitu vipya n.k.
Kwenye filamu fupi ifuatayo Jill Tarter anaongelea programu ya SETI na utafiti wao wa kutafuta civilizations nje ya sayari yetu:
Unadhani tuko wenyewe kwenye ulimwengu mzima? Au unaamini watu wa SETI watafanikiwa? Je, teknojia yetu inatupumbaza tu na kutupa 'kiburi'?
Kwa kuwa hakuna faida yoyote, hizi hela si zingetumiwa kutatua matatizo ya nishati kwenye sayari yetu?...Napenda kusikia mawazo yenu!
Tuesday, April 13, 2010
Watanzania tunaogopa Sayansi?
Takribani miaka miwili iliyopita watu kutoka kila kona ya dunia walikuwa wanazungumzia utafiti wa fizikia uliokuwa unaanza Geneva kutumia Large Hadron Collider (Picha halisi za vifaa na mashine zinazotumiwa zinapatikana hapa (virtual tour)). Ingawa sina takwimu zinazoweza kuniambia ni Watanzania wangapi walikuwa wanafuatilia au kutaka kuelewa nini kilichokuwa kinaendelea, nina uhakika ni wachache sana.Kwa kifupi, wanasayansi wanataka kutafuta na kuelewa asili ya tungamo (mass); nini hasa hukipa maada uzito?
Maada inajengwa na molecules; ambazo hujengwa na atoms; ambazo zina viini ambavyo vina nucleons (neutrons na protons). Nucleons nazo zina 'vikolombwezo' vyake. "Tatizo" hujitokeza pale unapoangalia tungamo la - kwa mfano - proton moja: proton ina tungamo la 938 MeV/c2 na vitu vitatu (quarks 'uud') vilivyomo ndani ya proton vina jumla ya tungamo la 11 MeV/c2 tu! Na mpaka sasa hivi hakuna ushahidi wa chanzo cha tungamo linalobakia (zaidi ya 925 MeV/c2). Kwa maneno mengine, huo utafiti unaoendelea huko Geneva ni juhudi la kutafuta jibu la hili swali.
Experiments za awali zilikuwa na matatizo ya hapa na pale, lakini wiki mbili zilizopita kulikuwa na mafanikio yaliyokuwa yanategemewa. Na mijadala inaendelea. Lakini katika kipindi chote hiki sikuwahi kuona au kusikia Watanzania wakiwa kwenye midahalo inayohusu huu utafiti na tafisi nyingine muhimu kwa ujumla. Mbona hata hatuulizi maswali? Je, tunadhani haya mambo hayatuathiri kwa njia moja au nyingine? Au hatuna watu wanaoweza kunyambua na kutusaidia kung'amua nini kinachoendelea?
Ifuatayo ni filamu fupi ya Michael Specter ambaye anazungumzia hatari ya jamii kutoipa nafasi sayansi kwa ujumla. Labda baadhi ya mambo ni mapya kwa Watanzania wengi wa kawaida, lakini tujue fika kuwa ndipo dunia inapoelekea. Inabidi tuulize maswali; hata kama huelewi kila kitu kuna uwezekano mkubwa watoto au wadogo zako wakaanza kudunduliza ujuzi wa kuwa wadadisi.
Nimekuwa nikisita kuandika kuhusu mambo kama haya kwasababu hayapewi kipaumbele kwenye jamii yetu kwasababu mbalimbali. Lakini wengi wetu tunajua nafasi gani vizazi vya watoto na wajukuu zetu vitakapokuwa ukilinganisha na wenzao kutoka nchi nyingine.
Kama unadhani mambo haya ni mazito sana, nenda kapumzike halafu rudi hapa kutoa mchango wako!
