Tuesday, June 15, 2010

African Hip Hop Thesis

Mimi kama mpenzi mkubwa wa Hip Hop, nimekuwa nikijaribu kuifuatilia kwa karibu tangia '2 Proud' alipokuwa anavuma na nyimbo kama 'Ni mimi, niko kwenye maikrofoni' na 'Madawa ya kulevya'. Safari ya Hip Hop Tanzania ni ndefu kiasi chake -- ila wengi mtakubaliana na mimi kuwa hatuna "kioo" (as in, standard) madhubuti cha kuangalia na kutath'mini mabadiliko yaliyoletwa na huu muziki wetu.

Mara nyingi mambo mengi tunayojadili kuhusu Hip Hop tunakuwa kama tuna speculate tu. Kwahiyo, tunayoongelea kwenye kijiwe hiki ni tofauti na yatakayoongelewa kwenye kijiwe kingine kutokana na sababu kadhaa.

Fid Q nadhani ameliona hilo na ameamua kufanya utafiti kuangalia Hip Hop kutoka Afrika -- utafiti huu wa kitaaluma utachunguza nini hasa kinachotokea kwenye ulingo wa Hip Hop, mabadiliko kwenye jamii yanayoambatana na Hip Hop, (bila kusahau) Hip Hop kama kitambulisho cha Vijana wengi sasa hivi.

Kilichonifurahisha zaidi ni kwamba anajua wapi pa kuanzia (kwasababu mambo ya utafiti yanahitaji maujanja, na kujua wapi pa kuanzia hurahisisha kazi); ataanza kuongea na wasanii ili kujifunza kama wanafikiri wana nafasi yoyote kwenye jamii.

Mimi binafsi nina maswali mengi mno. Lakini sasa hivi nitamuuliza Fid Q maswali machache tu kwanza ili aanze kuumiza kichwa:

1. Marekani inajulikana kama ndio chimbuko la Hip Hop, lakini sasa hivi inaonekana kama Hip Hop inaanza 'kurudi' Afrika (Soma makala kuhusu hili suala hapa). Je, kuna sababu za msingi au ni jambo la kawaida tu?

2. Wasanii wanajua maana ya Hip Hop? Wanaitumia ipasavyo?

3. Niliona filamu moja (documentary) inayozungumzia kufanana kwa maneno ya mitaani kutoka Marekani na Afrika Mashariki (ingawa lugha zitumiwazo ni tofauti). Kuna ukweli wowote ule?

4. Vipi kuhusu mambo yanayozungumzwa kwenye nyimbo mbalimbali. Sehemu mtu anapotoka (msanii) ina athari kubwa sana au ndogo kwenye nyimbo anazoimba? Au hutegemea zaidi mambo fulani mtu aliyopitia kwenye maisha yake binafsi? Ni sahihi kulundika wasanii kutoka Mwanza, Arusha au Dar kwenye kundi moja? Au tuangalie hadi vitongoji wanavyotoka?

5. Kuna baadhi ya wasanii kutoka Tanzania ambao wanaheshimika sana nje ya nchi ilihali bado wanatumia lugha ya Kiswahili kwenye nyimbo zao. Hii inakuwaje? Wengine wanatumia maneno kutoka Temeke!

6. Mabadiliko yanayotokea kwenye Hip Hop yanaakisi yanayotokea kwenye jamii? Au jamii huakisi mambo yanaongelewa na wasanii?

Nitaishia hapa kwa leo.

Ila kama una maswali zaidi au una maujanja yatakayoweza kumrahisishia utafiti huu, unaweza ukamtumia Fid Q barua pepe: cheusidawa (at) gmail (dot) com. Au unaweza ukatembelea blog yake (ina mipini yake karibia yote; cheki upande wa kulia).

Fid Q, Vijana FM inakutakia kila la kheri! Binafsi, nina uhakika kazi yako itawanufaisha wengi.

Makala nyingine kuhusu Fid Q zinapatikana hapa na hapa...

4 comments:

  1. Hamna noma. Endelea kuja hapa kijiweni!

    ReplyDelete
  2. Kati ya wanamuziki walio makini TZ, FID Q anaongoza. Big up kamanda, spice things up.

    ReplyDelete
  3. nasubiria kuona matokeo ya utafiti yatakuwa vipi, but all in all..hii poa sana, UCLA walikuwa na project kama hii ya kuona influence ya hip hop katika jamii through their musicology program..hongera Fid

    ReplyDelete