Tuesday, March 16, 2010

Fid Q - Bongo Hip Hop Star

Fareed Kubanda a.k.a Fid Q ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Hip Hop wenye uwezo mkubwa katika utunzi wa mashairi. Album yake mpya inayoitwa "Propaganda" haitakuwa na uchache wa vina na misemo, kwani fasihi simulizi ya Fid Q katika kughani niya hali ya juu. Fid Q kama wasanii wengine wa hip hop/ bongo flava, wameanza kuchanganya lugha, yaani kiingereza na kiswahili katika nyimbo zao. Msanii mwingine ni K-Lynn na nyimbo yake ya I am not a flirt. Hili ni jambo jipya kidogo, kwani mpangilio huu umezoeleka zaidi na wasanii wa genge wa Kenya. Nimejaribu kufikiria ni nini hasa kimepelekea sababu hii, na jibu moja nililojipatia ni, kutaka kupenyaza hip hop ya bongo katika soko la dunia.

Lugha ya kiingereza itaweza saidia watu wa nje waweza kuelewa na hapo hapo bila kuwapoteza wapenzi wa bongo hip hop wa nyumbani kwa kutumia kiswahili pia. Kitu kimoja ambacho bado sijaelewa ni kwanini album za hip hop Tanzania haziwezi kuuzwa kwenye itunes, ili kuwapa watu wa nje urahisi wa kuzinunua na hapo hapo kuwaongezea wasanii wenyewe kipato kwani mauzo yataongezeka. Kama nia ya uchanganyaji lugha nipanua wigo wa watu wanaokusikiliza na kupenyeza kwenye soko la dunia la mziki, basi kuna umuhimu pia kuuza album kupitia itunes.

Video yake yakitambo kidogo ya nyimbo "I am a Professional" inazidi kudhihirisha mpangilio mpya wa kuchanganya lugha mbili katika nyimbo za bongo hip hop/ bongo flavaI think its important we support local artists, because people like Fid Q have the ability and the skills like many of the US rappers, and even better than some of them. But like I said before, the idea of selling bongo hip hop albums on itunes is something that needs to be looked into. Look for Fid Q new album called "Propaganda" and listen to this guys word play skills.

Hii ni single mpya ya Fid Q Danger kutoka kwenye album yake ya "Propaganda"
To listen to more of Fid Q music visit his facebook

7 comments:

 1. Itabidi uandike nakala ya K-Lyinn pekee, maana'ke track imetulia (ila sijui ni picha tu ile, au?).

  Ok, umakini sasa! Naelewa lengo la Vijana wenzetu la kuvuka mipaka. Lakini wasisahau kuwa hawana budi kujaribu kudumisha vionjo ambavyo vitawatambulisha kama Watanzania. Itakuwa haina maana kwenda Nigeria halafu wazawa wanadhani unatoka Marekani.

  Kuna wasanii wengi wa Afrika waliofanikiwa kuvuka mipaka, hasa wa Afrika Kusini, Nigeria, na kwengineo. Lakini binafsi walionigusa ni P-Square. Ukiwasikia tu utajua hawa jamaa wanatoka Naija; na hata wanachokiimbia kinatoka Naija.

  http://www.youtube.com/watch?v=1_t8tBrZuqo

  ReplyDelete
 2. Jamaa akiendelea na word play hiyo hiyo ya Swanglish itamsaidia kupanua soko. Ila isiwe kusema kuwa wanamuziki wetu wa TZ wakitaka kutoka itabidi warap kwa kiingereza tu. Ninamfagilia jamaa fulani anaitwa Wakazi, jamaa anachipukia na kiukweli ninadhani akianza kutoa records zake mwenyewe atafika mbali. Kwani anaweza kuimba/rap kwa kiingereza na kiswahili. (search "Wakazi" on FaceBook). Originality sells too I think, look at Fally Ipupa. Jamaa anafagiliwa Afrika nzima na hata Ulaya na US ilihali si wote wanaelewa lingala au kifaransa - sahivi ana wimbo na Olivia wa G-unit.

  ReplyDelete
 3. unachosema ni kweli, Tanzania tungekuwa na kitu kama kwaito ya Afrika Kusini ingekuwa poa sana. Mpaka sasa sijapata jibu kwanini Xplastaz hawafagiliwa kwa ubunifu wao wa kuwa na kitu original, manake najua wanafanya vizuri nje ya bongo lakini bongo watu wamewang'ang'ania akina ali kiba..

  Huyo mshkaji wa Congo na Olivia safi sana. Alafu Wakazi yuko poa, ndo nimemkumbuka kuwa ndio yule aliyekuwa na beef na Beezy. Mwenye weza wasiliana na Fid Q aweze kutuambia inakuwa vipi na hii swanglish na nini kifanyike kuvuka mipaka ya kimataifa kwa uhakika...

  ReplyDelete
 4. I was thinking about this the other day. If I compare Jay-Z and Professor Jay, who would come on top regardless of language. I've listened to all, if not all of their albums. Hell...i'll even throw NAS in there.

  In my opinion i think Prof Jay can hold his own. He even seems more mature in my opinion. Its just my opinion. I could be wrong. What do you guys think?

  Eminem Vs Mangwair on free style battle on a P.Funk and Dre beat aiseee....Bongo tupo juu...

  ReplyDelete
 5. hahaha...Paul safi sana, nimependa hizo comparisons. Sijui sana kuhusu Jay-Z na Jay, lakini Mangwair vs Em, mhhh..acha tu, Em siku hizi ana-flow ya hatari, sikiliza Forever ya Drake, verse ya Em ni noma, hata kwenye BET Cipher, Em alitisha. P-Funk na Dre, interesting one, sema sisikii kazi nyingi za P siku hizi, sema huyu dogo Lamar...mhhhh!!, huyo sasa, Lamar na Dre au Lamar na producers wengine wa America...

  Kuna mshkaji enzi zile alikuwa anaitwa Hasheem a.k.a Bongo Psychological, sijui Paul ulishawahi kumsikia, huyo jamaa alikuwa anamashairi, manake kote kote alikuwa mkali, ngeli safi na kiswahili cha kamusini pia kilikuwemo..mimi bado natafuta nyimbo zake...

  ReplyDelete
 6. Kwenye kulinganisha watu nadhani mimi lazima nitakuwa biased tu. Kwahiyo nitatoa maoni yangu kidiplomasia hivi.

  Mimi binafsi, namuheshimu Prof. Jay na nadhani nyumbani hapewi sifa na heshima anayostahili. Jamaa anaandika mazee. Enzi zile 1998/9, kuna track moja kwenye albamu yake ya kwanza "Machozi, Jasho na Damu" (wimbo unakwenda kwa jina hilo hilo), nilibakia kutikisa kichwa tu. Yaani ulimgusa kila aina ya Mbongo.

  Kama Prof. angetoa Bongo Dar es Salaam leo hii, tungesema kamuiga Jay-Z (Empire State of Mind)!

  Mimi nashindwa kulinganisha watu, lakini kipimo changu ni 'longetivity'; mtu anavyobadilika kutokana na mabadiliko ya jamii au maisha yake binafsi na kuendelea kufanya kitu cha maana. Nadhani hata mimi nikiachwa na mitambo mizuri kwenye studio kwa miaka kadhaa, nadhani nitabahatisha 'hit' moja ya nguvu :).

  ReplyDelete