Friday, March 5, 2010

Nitoke vipi?

Siku ya Ijumaa ina utamu wake jamani, we acha tu. Hasa ukiwa umeridhika na kazi nzito na murua ya wiki nzima. Unaweza ukajikuta unaingia kwenye mawazo ambayo sio ya kawaida. Mimi hapa nilipo nasubiri mvua ipungue ili nianze safari ya kwenda nyumbani...ghafla, nakiangalia kitasa cha mlango wa ofisini. Nakiangalia kwa makini na naanza kujiuliza, hivi nani aligundua kitasa (cha mlango)? Mtu au watu waliogundua vitasa na funguo walikuwa wanafikiria nini? Kitasa ni kitu kidogo tu lakini nadhani kina historia kubwa kuliko ukoo wangu.

Baada ya kuzoea 'msisimuko' wa mwanzo wa weekend, akili inatulia kidogo na naanza kutafakari mwelekeo wa maisha yangu - kama kijana wa kawaida. Nini kitafuata baada ya kumaliza hiki kinachokula ubongo wangu kila siku?

Napitia forum ya Wanabidii, ambayo ina mijadala mizuri, na mawazo ya kuingia kwenye Siasa naona yananinyemelea baada ya kusoma kwamba Wabunge wa Tanzania wanategemea kupata kiinua mgongo cha shilingi za Kitanzania 15.3/= bn. Sijachapia - bilioni 15.3! Sidhani kama nitaelewa kusema ukweli. Na nitashukuru sana kamati husika za Serikali zikitoa takwimu kama hizi, zitoe maelezo au sababu za viinua migongo kwa wananchi pia.

Nitoke vipi kwenye Siasa na mimi nithaminiwe zaidi kuliko kitasa cha mlango tu?

Naona mvua imepungua na safari ya kwenda nyumbani itaanza punde. Wakati huo huo ubinadamu au mawazo yangu ya kawaida yanarudi baada ya kukumbuka matokeo ya kidato cha sita yaliyopita. Labda hizi bilioni 15.3 zipelekwe kwenye sekta ya elimu?

Ngoja niache kufikiria mawazo ya Siasa ili nisitibue weekend yangu. Weekend njema Vijana!

3 comments:

 1. Siasa ya Tanzania ni mchezo mchafu. Ninadiriki kusema. Kwahiyo kakaangu sidhani kama unahitaji uingia kwenye siasa ili uthaminiwe. Namna ya 'kutoka' kufahamu ni namna gani extreme-ultraviolet lithography (EUVL) inaweza kutumika kupanua uwanja wa sayansi na kubadilisha mwelekeo wa teknolojia.

  ReplyDelete
 2. aiseee..I hope i will not be an engineer for the rest of my life. I really do hope so. Mimi nisingependa mwanangu ahangaike kujaza financial aid forms kama sisi wakati wa university...eheheh

  kuna track ya "lolilo ft Prof Jay - Maisha"
  nimeipenda kwa kweli...kuna line lolilo anasema......"tunachakarika,tunachafuka...lakini maisha swata...yanakataaa,...yanakataaa...."lol

  ReplyDelete
 3. Sasa, tuwaache wanaotaka kuongoza nchi halafu tusubiri matokeo? Sidhani kama tutakuwa na hoja pale mambo yatakopaharibika; kwasababu hatukutaka kujitoa mhanga na kutengeneza nchi kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo.

  Au ubebaji box huku unatufumba macho? Kwasababu, mwishowe, nyumbani ni nyumbani tu. Na wengi wa walio nje ya nchi itabidi warudi tu.

  ReplyDelete