Tuesday, March 30, 2010

Katuni kutoka Afrika Mashariki

Naamini Vijana wengi ni mashabiki wakubwa wa katuni. Bila shaka utakuwa unakumbuka enzi zile jinsi kila Alhamisi ilivyokuwa ina raha yake. Nilikuwa sina budi kuibana hela ya matumizi shuleni ili ikifika Alhamisi niweze kununua nakala yangu binafsi ya gazeti la Sanifu! Kuna siku nyingine kama nina ziada ya jiti, nanunua makala mbili: moja ya kwangu mwenyewe na nyingine ni kwa ajili ya waazimaji (shuleni). Kuna baadhi ya wazazi ambao hawakupenda kuwaona marafiki zangu wakisoma Sanifu. Nilikuwa siwaelewi!

Kulikuwa na kurasa ambazo unaziangalia kwanza kabla ya kusoma vitu vingine. Sura ya wiki, Mwakipesile, Mzee wa Rivasi, Tolu, Ndani ya Nyumba (mambo ya misemo tata)...

Miaka imeenda na nimekuwa mtu mzima lakini sijaacha kufuatilia wachoraji maarufu. Niko kwenye juhudi za kuomba ruhusa na baraka za wasanii mbalimbali ili niweze kupost katuni zao hapa Vijana FM. Mpaka sasa hivi ni mchoraji mmoja tu, Zapiro kutoka Afrika Kusini aliyenipa ruhusa na baraka zake.

Kama una mawasiliano na Masoud Kipanya, tafadhali, itakuwa ni jambo la busara kumuomba awasiliane nasi.

Mchoraji mwingine maarufu ni Gado ambaye anafanya shughuli zake Kenya. Hapa ninawaomba wenzangu tutumie nguvu ya umoja ili tumsihi atupe ruhusa. Tembelea ukurasa wake wa facebook na ukiweza mwandikie e-mail. Juhudi zangu zimegonga mwamba! Pia, kama wewe ni mchoraji na unataka Vijana waone kazi yako usisite kuwasiliana nasi.

Nia na madhumuni hasa ya kuzianika katuni zao hapa ni kuanzisha mijadala ya aina mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya katuni za zamani kidogo kutoka kwa Gado (Chanzo):2 comments:

  1. boss, shukrani. bado tunamsubiri mwenywe Bwana Kejo kule bongo and more inshallah. nadhani picha zina experience kubwa sana kuliko neno ama text. hapo london gazeti mengi hawana katuni siku hizi, jamani siwezi kusoma text shuleni, nyumbani, na kila sehemu bwana! lazim tutafute wachoraji kutoka mbalimbali ili mimi mwenywe nta weza ku cheka kidogo kusu vishuli za dunyani :)

    asante tena.

    ReplyDelete