Wednesday, March 3, 2010

MTV's Staying Alive...Inahitaji Pongezi

Ijumaa moja nilikuwa nimetulia tu nyumbani kama kawaida nikisoma Robbo blog, kufuatilia matukio mbalimbali na kujiandaa na mechi zilizokuwa zinafuata kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. Kwangu hiyo ni burudani tosha baada ya pilika pilika za wiki nzima kwenye maabara.

Rafiki yangu akanitumia 'link' ya website ambayo ilikuwa ina film 'Shuga', iliyotengenezwa Kenya kwa hisani ya kampeni ya MTV's Staying Alive. Aliniambia tu, 'Hii ni kali!' Kama kawaida yangu nilisita kidogo; yaani niache kusoma Robbo blog halafu niangalie kitu ambacho nimekuwa nikikisikia tokea 1996 (elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi/Ukimwi)?

Kabla ya kulala nikaamua kubofya ile 'link', kuangalia kilichopo huku nikiuvuta usingizi taratibu. Nilikuwa nimechoka lakini baada ya kuangalia film kwa dakika kadhaa usingizi ulitokomea. Nikaiangalia kwa makini film nzima na ujumbe nikaupata. Ni film ya zamani kidogo lakini ujumbe wake unamgusa kila kijana, hasa wale ambao wako vyuoni.

Ukiacha ujumbe uliokusudiwa kuna mambo mengine mengi ambayo yatakufumbua macho. Wale ambao wana ndoto au mipango ya kuingia kwenye fani ya utengenezaji, uongozaji wa kurekodi, uigizaji na pia utangazaji wa film nadhani watajifunza vitu viwili vitatu.

Ni film ya zamani kidogo na watu wengi labda wameshaiona, lakini nimeona sio vibaya kuianika tena na kuwapa ukumbi Vijana kuijadili.Shuga Episode 1 from mtv staying alive on Vimeo.Shuga Episode 2 from mtv staying alive on Vimeo.Shuga Episode 3 from mtv staying alive on Vimeo.Shuga Behind The Scenes from mtv staying alive on Vimeo.

6 comments:

 1. Mimi nilivutiwa sana na quality ya hiyo film. Kwa kweli wenzetu wamepiga hatua.Kwa upande wa hiyo filamu ina mafunzo mazuri.

  Ingawaje tumefundishwa elimu ya virusi vya ukimwi tokea enzi za shule ya msingi, bado idadi ya waathirika inazidi kuongezeka. Mbaya zaidi ni kwa watu wa vyuo vikuu ambao ni taifa la leo.

  Kwahiyo ni muhimu tuwe tunakumbushwa mara nyingi iwezekanavyo.Mimi kama mtanzania huwa najisikia vibaya sana ikifika tarehe 1 desemba ya kila mwaka.

  Hivi hizo takwimu za waathirika wa ukimwi kutoka WHO huwa ni za kweli au? Manake kuna mwenzangu aliwahi kuniambia kuwa, wakusanyaji wa takwimu huwasilisha idadi sisizo za kweli ili kuyawezesha mashirika yako na NGO's wapate misaada mingi ( hela ) ili wajinufaishe wenyewe.

  ReplyDelete
 2. Hii tamthilia niliipenda nilipoitazama. Mara nyingi wengi wetu tunakuwa na mapepe katika swala hili la ngono. Tunajisahau na tunaingia peku peku bila ya kutafakari. Ukimwi ni hatari aise, hata sisi tulio huku Ulaya, kirusi kipo kinatapakaa.

  Paul, kuhusu takwimu. Mara nyingi takwimu za kuaminika zinatoka katika mashirika makubwa kama WHO. Ndio maana wanasayansi wengi wana'quote namba za WHO katika 'paper' zinazohusu magonjwa. Takwimu za NGO mara nyingi zina utata, for obvious reasons.

  Joji

  ReplyDelete
 3. Mara nyingi ukiangalia hizi tamthilia zetu lazima kutakuwa na kasoro za hapa na pale. Kwa upande wa sanaa, sioni walipoteleza.

  Mi nilishtuka kidogo; labda nazeeka..Yaani vijana maisha ndio 'mkuku' kiasi hiki. Wazazi wakiona hii nadhani watashikwa na bumbuwazi (vijana kufanya mambo kama haya). Vipi kuhusu uhalisi wa hii tamthilia? Hawajalenga tabaka fulani tu?

  ReplyDelete
 4. Steve umegusa patamu. Hii tamthlia inagusa hasa hasa vijana wa mjini ambao wana access na anasa za kileo. Ingependeza kuwepo na documentary zenye kuonyesha uhalisia wa jinsi mambo yalivyo vijijini na miji midogo. Je, kondom zinapatikana kiurahisi kule kwetu kijiji cha Katerero, au Singida ndani ndani?

  ReplyDelete
 5. hii tamthilia safi sana, nimeiangalia mpaka sijaichoka..hah!!. Kwakweli imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, hakuna chembe ya ubabaishaji. Nadhani watengeneza filamu za bongo inabidi waangalia ubora wa utungenezaji huu, kutoka kwenye picha mpaka uandishi, safi sana. Kusema ukweli vijana sote ni sawa kila kona ya dunia, manake hata ukiangalia tamthilia za mtv stay alive za nchi nyingine, ni mambo yake yake tunayoyaona miongoni mwa sisi vijana wa tanzania. Kuna mtu alisema, ujana kama maji ya moto, hivyo tuwe waangalifu.

  ReplyDelete
 6. mhh..kuhusu swala la ukimwi...kuna documentary moja ya CNN 'Planet in Peril:Battle lines' kuna part wanaongelea jinsi magonjwa na wanyama pori.

  http://video.google.com/videoplay?docid=4844687588840076520&ei=g1CRS6LpN9Cr-AaU17m-Ag&q=planet+in+peril&hl=en#

  It looks at the bigger picture abt nature, endangered species...

  ReplyDelete