Wednesday, March 17, 2010

Peer2Peer Tutor, na sisi Je?

Leo nitaendelea na pale nilipoishia na ile changamoto ya kwanini na sisi tusianzishe Khan Academy zetu. Jambo la elimu na ujasiliamali linawezekana, na Erik Kimel anadhihirisha hilo na kampuni yake ya peer2peer tutor. Hoja yangu muhimu ni kujaribu kuboresha ufundishaji kwa kutafuta mbinu ambazo zitawezesha elimu kutolewa kwa ubora, ufanisi na kufurahisha. Matokeo mabaya ya mitihani ni moja ya udhibitisho kuwa wanafunzi hawaelewi wafundishwacho madarasani. Sasa kwakuwa kubadili mfumo mzima wa elimu ni kitu kigumu, hivyo basi tunaweza kuanzisha mradi kama wa Erik Kimel.

Jambo la pili, ninalozidi kulipigia kelele ni kujaribu kupata watu wenye uwezo na kuwashirikisha katika kuboresha namna za ufundishaji. Mimi ninaamini kuna wanafunzi wenye uwezo kiakili na wenye mbinu nzuri lakini hawajapewa motisha kutaka kuwa walimu. Hivyo basi, mradi kama peer2peer tutor, ambao utasaidia vijana kuwa wajasiliamali hapo hapo wakisaidia vijana wenzao, tuupe kipaumbele. Wazo la Kimel ni zuri sana, kwani hata mimi naamini, muda mwingine vijana tunaelewana na kujuana sisi wenyewe zaidi ya walimu wanavyotujua na kutuelewa. Sasa baada ya kusema yote hayo, mimi natoa changamoto kwa vijana wenye uwezo, kufikiria kuanzisha kitu kama peer2peer tutor. Jamani ujasiliamali na elimu ndio kama hivi, basi tusipitwe wakati uwezo tunao.

Kimel’s idea is a great one, and one that should motivate youths of Tanzania who have the knowledge and ability to teach to do the same. This is a great example of how entrepreneurship and education can go hand in hand without colliding. I think something like peer2peer tutor in Tanzania will be able to do two things. First, it will attract the youths with the knowledge and ability to teach, people like Khan of Tanzania, to help their fellow Tanzanians. I am talking about people who have the real passion for education but don’t want to get mixed up with the Tanzanian education system which is not so great in so many ways, just to say the least.

Secondly, this is a great entrepreneurship opportunity where people will help others and at the same time make money while doing so. Since Tanzania doesn’t have enough teachers, and even those few teachers that we have not all of them are competent, so here is the challenge for my fellow youths of Tanzania who have the knowledge and the passion for education to do what Kimel has done.

peer2peer tutor on cnn

No comments:

Post a Comment