Swala la ujasiliamali linakwenda bega kwa bega na ubunifu, na ubunifu unachangiwa kwa namna moja au nyingine na elimu. Tukikubali kuwa ujasilimali, elimu na ubunifu vinauwiano wa karibu, tutaanza kuona kwa ukaribu nyufa ambazo zinazozorotesha maendeleo katika elimu Tanzania na ujasiliamali kwa ujumla. Elimu inayotolewa haina changamoto ya kuchochea maendeleo. Hivi leo katika zama hizi za sayansi na teknolojia ungetegemea kuona tunatumia maendeleo ya kiteknolojia kukuza ubunifu, lakini ndio kwanza tunazidi kung’aa macho.
Sasa ni wapi ninakwenda na hayo yote niliyosema, ni hivi yote haya yanalenga maswala mawili, kwanza elimu na teknolojia na pili ubunifu ndani ya ujasiliamali kwa kutumia teknolojia. Hili tunaweza kuliona katika video ifuatayo ya huyu bwana Khan ambaye anatumia youtube kuelimisha dunia. Sasa Khan ni mfano wa jinsi gani teknolojia inaweza kuboresha elimu/ ufundishaji na jinsi ambavyo walimu wanaweza kufanya kama alivyofanya Khan na kutengeneza pesa kwa madarasa watakayo weza kuweka mtandaoni. Sio kazi rahisi lakini hakuna mwanzo mrahisi kwa kawaida.
Madarasa hayo siyo lazima yawe ya hisabati, sayansi, n.k bali madarasa ya sanaa, kwa mfano namna ya kuchora tingatinga. Internet imetupa uwezo wa sisi kuweza kuwa wabunifu bila mipaka lakini bado tumeng’ang’ania ku-surf tu. Mfumo kama huo wa Khan Academy unaweza boresha sekta ya elimu na jinsi tunavyo elimisha vijana. Kwanza, itawapa wale watu wenye uwezo kuelimisha lakini hawataki kujihusisha na mfumo dhaifu wa elimu ya Tanzania nafasi ya kusaidia. Pili, watu wataweza kujiwezesha kiujasiliamali kwa kutumia mbinu kama ya Khan. Najua kutakuwa na matatizo ya hapa na pale, hasa ukizingatia miundo mbinu yetu bado inamatatizo, lakini ni swala ambalo siyo baya kulitupia macho na kuanza kulifanyia kazi.
Sasa mimi nawaachia vijana wenzangu changamoto hiyo. Tanzania bado tupo nyuma, na wenye uwezo tuanze kuanzisha Khan Academy zetu japo kusaidia wale ambao hawakupata bahati au nafasi ya kwenda shule kwa sababu moja au nyingine. Wakereketwa mpoooooooooooooo…kazi ni kubwa na safari si fupi, na maendeleo ya Tanzania yapo juu ya migongo yetu vijana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Bado nimeshikwa na BUMBUWAZI baada ya kuitembelea website ya Khan [ www.khanacademy.org ]!
ReplyDeleteNina uhakika maisha yangu chuoni yangekuwa rahisi mno kama ningekuwa naijua hii Academy. Wanafunzi wana bahati sana siku hizi kutokana na info/ujuzi/habari zinazopatikana kwenye mtandao. Ila Vijana wangapi watapata hii info na kuitumia ipasavyo? Kutokana na desturi zetu za utumiaji wa mtandao kila mtu atakuwa ana jibu lake binafsi.
Shukrani sana Bahati! Nina uhakika Vijana wengi wakijua hii ishu mahudhurio kwenye madarasa ya tuition yatapungua kwa kasi ya ajabu, na utakuwa kama umeanzisha vita na walimu (indirectly).
Kama vitu kama hivi havitupi motisha ya kutosha basi ujue tuna gundu...
Boss, this article ni muhimu sana. The boundaries around earning an education are breaking fast, and as Mr. Khan shows, some people value knowledge for just that, knowledge. Sio pesa ama recognition etc.
ReplyDeleteAnother example where education is being informalized is with Open Source software. Check out how Ubuntu, one distribution of the Linux operating system, is being translated into Swahili:
http://ubuntuforums.org/showthread.php?t=490044
Asante chief. Look forward to seeing more examples.