Wednesday, March 31, 2010

Just Google him!...Webiro 'Wakazi' Wassira

Kuna wakati wasanii nyumbani walikuwa wanategemea vituo vikubwa vya redio - hasa Clouds FM - kuamua mafanikio ya kazi zao. Kwa maneno mengine, kama kazi yako ikikubaliwa na ikachezwa vya kutosha na Clouds FM basi unapata uhakika wa kupata shows. Wale ambao nyimbo zao zilikuwa zinatupwa kapuni ilibidi warudi wajipange upya au kuhamia kwenye fani nyingine.

Lakini kuna Vijana ambao wamefikiria na wakaona mbali zaidi.

Siku moja nilitumiwa nyimbo inayoitwa 'Mshindi' na mdogo wangu anayesoma India. Akaniambia tu, "msikilize mbongo huyo." Nilikuwa natumia headphones uchwara, lakini baada ya beat kuanza ilinibidi nihamishie mambo kwenye spika kubwa! Nikarudia kuusikiliza mara kibao na nikaanza kufanya utafiti ili nijue nani hasa anayeghani...


Jina: Wakazi!...Nyumbani: Ukonga, Dar es Salaam!...Makazi: Chicago!

Kusema ukweli sikuamini jinsi ilivyokuwa rahisi kupata habari na taarifa zote za Wakazi aka Swagga Bovu; bila kusahau nyimbo nyingine nyingi nilizoweza kuzisikiliza kwenye mtandao.

Wakazi anajishughulisha na mambo mengine lakini ana mapenzi makubwa na Hip Hop. Ukiacha utundu wake wa kucheza na maneno ya lugha ya Kiswahili na Kiingereza, inaonekana amefikiria mbali. Ameona nini kinaendelea kwenye teknolojia (hasa mtandao) na akaamua kuelekeza juhudi zake zote kwa kujitangaza kupitia twitter, facebook na myspace. Na wiki hii amezindua tovuti yake. Idadi ya watu wanaofuatilia kazi zake za muziki inazidi kukua na hii inaasharia kuwa juhudi zake zinaanza kuzaa matunda.

Sitashangaa akianza 'kuwapiga bao' wasanii ambao tayari wako juu kwenye vituo vya redio Bongo pindi mtandao wa fibre optic utakapoanza kutumiwa na watu wengi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Kama wahenga walivyosema, "Chema chajiuza, kibaya chajitembeza."

Sasa hivi ana Mixtape ya Ukweli Vol. 1* ambayo imeanza kutapakaa kwenye mtandao (click here to download). Na yuko studio akirekodi mixtape yake ya pili na album yake ya kwanza.

Wale ambao wako Dallas, Texas, Wakazi atakuja kuwakonga nyoyo zenu kwenye weekend ya Pasaka. Kama unataka kujua mambo mengine zaidi...Just Google him! Au mwandikie e-mail: wakaziwavina (at) gmail (dot) com.


*Quote from the mixtape review: "If I start quoting his best punchlines or one-lines, then it won't be an ending process as the whole mixtape got those, you can peep wordplay here 'Kimziki wewe ni Cheater (Chettah), unafanana na duma!'"

3 comments:

 1. safi sana hii. Kweli kuna watu kwenye Bongo Flava wameanza kutumia mtandao kujiendeleza. However, huyu mshkaji yupo states hivyo ni rahisi zaidi kutokana na ma-exposure, ukilinganisha na hali halisi ya bongo, mara umeme, mara kulipia internet cafe, hivyo naelekewa kwanini mambo kama haya huwawiya wengi ugumu.

  But all in all, hivyo nilivyotaja visiwe visingizio kwa wasanii kutumia technolojia to their advantage.

  Huyu jamaa nilianza kumsikia kupitia beef yake na Beezy. Hivyo my first impression juu yake haikuwa nzuri, kwanini nasema hivyo. Mimi hip hop ya bongo bado naona ni changa (najua ni miaka sasa bado tunasema changa), hivyo swala la beef halikunivutia kwani sikuona ni vipi beef zinaweza jenga sanaa, hasa hii ya bongoflava ambayo bado inajivuta vuta.

  Mimi bado ninakasumba na wasanii wa bongo hip hop ambao wako too westernized, thats just me, ndio maana kwenye makala iliyopita, pamoja nilikuwa somewhat critical juu ya Xplastaz lakini nawaheshimu sana kwa ubunifu wao.

  Wakazi na mwelekeo mzuri, na nimesikiliza baadhi ya kazi zake nikafurahia. Sasa changamoto kwa masanii kama yeye ambaye yupo nje, na kama exposure ameshapata sana, je nini anafanya kukuza mziki wa bongoflava/ hip hop bongo global, na ni nini kama yeye msanii aliyopo ugaibuni anachofanya tofauti na wasanii wa nyumbani ambao exposure yao ni ndogo.

  Wasanii waliopo nyumbani wanataka kutoka na kuwa global, je hawa kama Makazi ambao wako global tayari, nini mchango wao. Juzi UK kulikuwa na mkutano wa Diaspora, nadhani hili swala la Diaspora lingetazamwa kwenye huu mziki wa bongo flava. Jamani tusaidiane, safari ni ndefu, na sidhani kama itakuwa rahisi, kwani kidole hakiuwi chawa..basi tusaidiane.

  ReplyDelete
 2. Shukrani Mzee Critique!

  Kuhusu visingizio, mzee umenena. Nitatoa mfano hapa halafu niambie ugumu uko wapi kwenye utekelezaji. Nitaanzia chini kabisa!

  Mimi ni mmoja wa wanamuziki wa kikundi fulani cha Hip Hop/Bongo Flava. Naamua kujaribu kujitangaza kupitia mtandao. Sina utaalamu sana wa kompyuta na wala sijui mambo ya twitter, facebook au myspace.

  Naamua kuulizia watu na kujifunza kutumia vitu/tovuti nilizozitaja hapo juu*; inanibidi nifanye kozi ya kompyuta, hasa matumizi ya mtandao. Baada ya kupata mwangaza naamua kuwashawishi wenzangu (kundi langu zima la Hip Hop/Bongo Flava) kutumia mtandao kujitangaza. Kwasababu sina nyimbo nyingi za kutosha kuwavutia watu wengi, inaniwia kuungana na wenzangu kuanzisha kitu kama:

  www.myspace.com/Ubungo-Kisimani

  Nina-upload nyimbo zetu na kuanza kuitangaza tovuti yetu kwa nguvu zote (hasa vyuoni na mashuleni; facebook n.k.). Nikienda kwenye mahojiano ya vituo vya redio, shows..I just drop the line "Ubungo-Kisimani tunapatikana hapa bla bla bla".

  Ninaamini kama una nyimbo nzuri, utafanikiwa tu! Hautakuwa una budi kupigana vikumbo na DJs kila siku kuwaomba wacheze nyimbo yako.

  If you are too busy with other things like recording, tours etc., just snatch some kid off facebook and hire him/her to do everything for you part-time. Updating the myspace page wouldn't take more than 5 hours a week. Unampa mshiko wake kama laki tatu kwa mwezi...No scratch that! There are geeks out there who will be willing to do it for FREE (unawapa free passes kwenye concerts zako)!

  Chema chajiuza, kibaya chajitembeza. Angalia nyimbo ya Jay Msilie..imetapakaa kwenye mtandao!

  Kwahiyo, pongezi kwa Wakazi! Watu watajifunza kutoka kwako.

  ReplyDelete
 3. A promising talented artist-MJ

  ReplyDelete