Raghava KK is an artist who started by drawing cartoons in the classroom. Listening to him and see what he has done, you’ll agree with me, his pencils & paint brushes are mightier than the sword. One thing that really impressed me with Raghava is his creativity, and how his art evolves and transforms, while still maintaining its originality.
Secondly, how he collaborates with different type of artists to revolutionize his own is just so impressive. I hope young artists will learn not to limit themselves, kwani ubunifu kama huu ndio unao kosekana kwa wasanii wengi wa Bongo Hip Hop/ Bongo flava na hata aina nyingine za sanaa.
Showing posts with label Cartoons. Show all posts
Showing posts with label Cartoons. Show all posts
Tuesday, June 15, 2010
Tuesday, May 25, 2010
Siasa na Vikaragosi…

Leo hii nimekumbana na habari hii inayohusu kipindi hiki kinachoitwa Za Newz cha Afrika ya Kusini. Kipindi hiki kinafanana na ze comedy cha Tanzania, sema wao wanatumia vikaragosi na wamezamia zaidi kwenye ulingo wa siasa.
Kipindi kama hiki cha ze newz kina nafasi kubwa sana kwenye jamii zetu, hasa katika kuelimisha wanajamii maswala ya kisiasa. Tanzania tukiwa bado na mwamko mdogo katika siasa, vipindi kama hivi vinaweza kuongeza changamoto na mwamko wa kisiasa, hasa miongoni mwa sisi vijana. CCM wamenza kufanya hivyo kwa kutumia wasanii wa bongoflava, mfano ni katika kampeni yao ya mimi nimechangia, naomba na wewe uchangie pia.
Vyombo vya habari bado vinakazi kubwa kuhakikisha wananchi wanajihusisha na maswala ya kisiasa. Kupiga kura ni namna moja tu ya kujihusisha na siasa, lakini je tunazifahamu itikadi za wagombea vizuri. Lazima tujue katiba ya vyama tunavyotaka kuvipigia kura. Sasa kipindi kama Za Newz kinajitahidi kusogeza jamii karibu na maswala ya kisiasa kwa kutumia njia ya kukejeli na kuchekesha. Mimi ninadhani hiyo ni njia nzuri ya kuvuta jamii hasa vijana, na kuwapa habari juu ya maswala mbalimbali ya kisiasa.
Uchaguzi mkuu wa raisi na wabunge ndio huo unakuja, lakini je, sisi kama wapiga kura tumejiandaa vyakutosha, au tunaenda tu kupigia kura wale wagombea wenye sura zenye mvuto na matabasamu mazuri?
Tuesday, March 30, 2010
Katuni kutoka Afrika Mashariki
Naamini Vijana wengi ni mashabiki wakubwa wa katuni. Bila shaka utakuwa unakumbuka enzi zile jinsi kila Alhamisi ilivyokuwa ina raha yake. Nilikuwa sina budi kuibana hela ya matumizi shuleni ili ikifika Alhamisi niweze kununua nakala yangu binafsi ya gazeti la Sanifu! Kuna siku nyingine kama nina ziada ya jiti, nanunua makala mbili: moja ya kwangu mwenyewe na nyingine ni kwa ajili ya waazimaji (shuleni). Kuna baadhi ya wazazi ambao hawakupenda kuwaona marafiki zangu wakisoma Sanifu. Nilikuwa siwaelewi!
Kulikuwa na kurasa ambazo unaziangalia kwanza kabla ya kusoma vitu vingine. Sura ya wiki, Mwakipesile, Mzee wa Rivasi, Tolu, Ndani ya Nyumba (mambo ya misemo tata)...
Miaka imeenda na nimekuwa mtu mzima lakini sijaacha kufuatilia wachoraji maarufu. Niko kwenye juhudi za kuomba ruhusa na baraka za wasanii mbalimbali ili niweze kupost katuni zao hapa Vijana FM. Mpaka sasa hivi ni mchoraji mmoja tu, Zapiro kutoka Afrika Kusini aliyenipa ruhusa na baraka zake.
Kama una mawasiliano na Masoud Kipanya, tafadhali, itakuwa ni jambo la busara kumuomba awasiliane nasi.
Mchoraji mwingine maarufu ni Gado ambaye anafanya shughuli zake Kenya. Hapa ninawaomba wenzangu tutumie nguvu ya umoja ili tumsihi atupe ruhusa. Tembelea ukurasa wake wa facebook na ukiweza mwandikie e-mail. Juhudi zangu zimegonga mwamba! Pia, kama wewe ni mchoraji na unataka Vijana waone kazi yako usisite kuwasiliana nasi.
Nia na madhumuni hasa ya kuzianika katuni zao hapa ni kuanzisha mijadala ya aina mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya katuni za zamani kidogo kutoka kwa Gado (Chanzo):

Subscribe to:
Posts (Atom)