Friday, June 4, 2010

Uwanja wa Fisi

Na Lars Johansson (with English subtittles)

Kifuatacho ni kisa cha dada Elisa kutoka Uwanja wa Fisi. Nadhani wengi wetu tumeshaiona hii filamu, lakini nimeona sio vibaya nikiipost tena hapa kwa ajili ya wachache ambao hawajawahi kuiona.Pia, timu ya Lars imetengeneza filamu nyingine kama hizi nyingi tu ambazo zinajadili matatizo mbalimbali -- kuhusu umaskini, vifo vya watoto wachanga, matatizo yanayowakabili wavuvi wa Ziwa Viktoria n.k. Tutazipost documentaries zote hapa.

Uzuri wa filamu hizi ni kwamba Lars (na wahusika wengine) wanaenda sehemu husika na wanawaacha wananchi watuambie hadithi zao kama zilivyo. Hii ni tofauti na watengenezaji wa filamu kama hizi ambao wanajaribu 'kupindisha' ukweli ili kujaribu kuwasilisha ujumbe wanaotaka.

Ili kurahisisha jinsi ya kuzitafuta hizi filamu hapa Vijana FM, filamu za aina hii (zilizotengenezwa na Lars) nimeziongezea label ya "LARS". Kwahiyo cha kufanya ni kubofya neno "Lars" tu kwenye orodha ya categories iliyopo kulia.

2 comments:

  1. mmmmh, kusema ukwel mmenigusa mpaka nimetoa chozi. tatizo kubwa linaletwa na viongozi wetu tunaowachagua kusaidia mambo kama haya lakini wao wanaishia kujinufaisha wenyewe, Eliza Mungu yupo na atakusaidia japokuwa mda wote nilikuwa natoa machoz ila sikusita kutabasam ulipotabasam... Love you Eliza

    ReplyDelete
  2. Ndio ukweli wa mambo.

    "watu wanauza nyuchi mpaka shilingi 200, 300.."

    Duu!

    ReplyDelete