Tuesday, June 8, 2010

Zum zum zum...

Lyrics:

Zum zum zum,
Eeeeh mama nyuki lia we.


Zum zum zum,
Eeeeh mama nyuki lia we.

Toka mbali, kutafuta, ua zuri, la maua,
Zum zum zum,
Eeeeh mama nyuki lia we.Haya, wenzangu mnakumbuka nyimbo gani? Maana'ke mkiniachia mwenyewe niendelee, blog nzima itajaa:

Mabata madogo dogo, yanaogeleeaa!
Katika shamba zuri la bustani!
Yanapenda kulia,
kwaa kwaa kwaaa kwaaaa kwaaa kwaaa!...

Utu uzima dawa, jamani. Kama ingewezekana kurudi utotoni...

Shukrani kwa da' Subi (sio kwa nyimbo! - bali kwa kutuonesha wapi pa kuzipata videos kutoka Bongo).

4 comments:

 1. This comment has been removed by the author.

  ReplyDelete
 2. Sasa sasa ni saa ya kwenda kwetuuu
  Kwaheri mwalimu...kwaheri...tutaonanaaa Keshooooo

  (Verse 2)
  Sasa sasa ni saa ya kwenda kwetuu...
  Kwaheri mwalimu...kwaheri...tutaonanaaa Keshooooo
  .
  .
  .
  .
  .
  .

  ReplyDelete
 3. aaa, sisi tulikuwa twaimba hivi:
  Maua mazuri yapendeza x2
  Ukiyatazama, utachekelea,
  Hakuna hata moja lisilopendeza.

  Zuuum zuum zuum, we Mama nyuki lia we x2
  Toka mbali kutafuta, ua zuri kwa chakula,
  Zuuum zuum zuu, we Mama nyuki lia we.

  Tujioshe mwili mzima, twende safi shuleni x2
  Meno tusafishe pia, nguo tufue x2
  Na kagele keupe, mwalimu anapenda x2
  Hii ndiyo afya tunayofunzwa shule x2

  ReplyDelete
 4. Watu hawasahau hata neno moja! Mna tapes za hizi nyimbo kwenye makabrasha yenu?

  ReplyDelete