Saturday, June 5, 2010

Tovuti ya Wahapahapa Na Sanaa..Leo hii sanaa bado haijapewa heshima na kipaumbele kama inavyotakiwa, pamoja na sanaa kuwa kioo cha jamii. Tovuti na blog zimeanza kumea kama uyoga, lakini chache zimekuwa zikitetea nafasi ya sanaa katika jamii na haki na umuhimu wa wasanii ndani ya jamii.

Wahapahapa ni moja ya tovuti ninazoweza kusema zimejikita katika sanaa, siyo kuishia kuzungumzia sanaa tu. Kitu kilichonifurahisha na tovuti ya wahapahapa, ni kuwa wameweka michezo ya kuigiza ya redio katika tovuti yao. Hii inawapa fursa hata walio mbali kufaidi sanaa hii kongwe iliyopewa kisogo kutokana na ukuaji wa utandawazi. Nadhani kizazi cha enzi zile tunaweza kukumbuka ile michezo ya akina marehemu Pwagu na Pwaguzi katika redio ya Taifa, RTD.

Tembelea tovuti hii ya Wahapahapa na sikiliza michezo hiyo ya kuigiza na pia kujisomea mambo mengi mengineo ya kuelimisha kupitia sanaa.

No comments:

Post a Comment