Friday, June 4, 2010

Hadithi fupi

Kwa wale ambao walikuwa wanafuatilia hadithi fupi hapa Vijana FM (unaweza ukazipata hadithi za awali hapa), nataka kuwataarifu kuwa zoezi la kuzipost hapa litasitishwa kwa muda. Huu uamuzi unatokana na ushauri niliopewa na baadhi ya wasomaji, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwa naangalia kama kuna uwezo wa kuzikusanya na kutoa kitabu hapo baadae (kama nikipata nafasi hiyo).

Kitabu (kitaitwa "Kelele za Ukimya - kutoka Uswazi") kikikamilika nitawataarifu na nitapost baadhi ya hadithi hapa . Wakati huo huo naelewa kuwa wahusika wanaweza wakakataa kuchapisha kutokana na mambo ninayoongelea na sababu nyingine wa kadha. Lolote litakalotokea, utapata fursa ya kuzisoma -- iwe kutoka kwenye kitabu, hapa Vijana FM, forums n.k.

Nawatakia siku na kazi njema!

__

SN.

2 comments:

  1. uamuzi bora kabisa. kila la heri

    ReplyDelete
  2. Shukrani sana, John! Bila nyie hata nisingefikiria kuandika kitabu.

    ReplyDelete