Wengi wetu tumesikia simulizi za kusisimua kutoka kwa wazazi wetu pindi walipokuwa jeshini (National Service). Nyingi zinahusu shida, uvumilivu, ufanisi na uzalendo. Ingawa kuna waliochukia maisha magumu waliyoyapata walipokuwa jeshini, wengi wao wanakumbuka kipindi hicho kwa tabasamu. Binafsi mama yangu anasikitika kuwa vijana wa leo hatupitii kimbembe kama alichopitia yeye baada ya form six kwa mwaka mmoja pale JKT Ruvu.
Mpango wa National Service ulianzishwa na Mwl. Nyerere katikati ya miaka ya 60 kwa nia ya kujenga taifa lenye watu wazalendo, jasiri, werevu na wakakamavu. Mchakato huu ulikuwa wa lazima kwa wanafunzi wote wanaomaliza shule ya sekondari kwenda katika kambi za jeshi na kupitia mafunzo mbalimbali ya kijeshi na kielimu kwa mwaka mmoja. Mpango huu ulifutwa mwaka 1992, na hivyo kufanywa wa hiari.
Nchini Tanzania, kuna mjadala umejitokeza kuhusu kurudishwa kwa mpango wa National Service kwa vijana wa sasa. Je, itakuwa vibaya tukirudisha mchakato huu kwa wanaomaliza sekondari kutumikia taifa kabla ya kujiunga na chuo au sekta binafsi? Simaanishi tuwe na national service ya kijeshi, la hasha, bali tuanzishe mpango kwa ajili ya wahitimu wa sekondari utakaoweza kuwapeleka vijana wetu vijijini kufundisha masomo kama hisabati, na lugha kwa kipindi cha miezi 6-12. Au hata kuwatumia vijana hawa katika hospitali zetu - kwenye awareness campaigns za ukimwi/malaria vijijini, au kuwatumia kwenye vituo vya kilimo, vituo vya wazee/walemavu/watoto yatima na hata kwenye mabenki. Ilimradi tu mchakato huu usiwe wa kitumwa, au mateso bali uliojaa elimu mbadala wa vitendo ili kujenga taifa imara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
In Tanzania one normally finishes Form 6 at 20 or 21. An additional year in such a scheme before University is a waste of time. I'm just sayin.
ReplyDeleteanon1.
ReplyDeleteIt would be good if we look at the benefits for the common good and not at individual level benefits. Umri kitu gani?
Mi' naona irudishwe tu, lakini nitawaomba wahusika wasifanye hii kitu ni kupiga gwaride tu. Namaanisha wawafundishe Vijana kuwa responsible kwenye jamii; mambo kama ya kujitolea, kutembelea vituo vya watoto yatima, kufundisha watoto n.k. (kama uliyoyataja mwandishi). Maana'ke Vijana wanadhani mambo ya kujitolea kwenye jamii ni wajibu wa watu maarufu tu.
ReplyDeleteMara nyingi watu huona kitu kibaya kwenye tarakilishi zao, husikitika tu bila kuguswa au kuitikia mwito wa kuleta mabadiliko... Na hii inatokana jinsi tulivyolelewa, labda?
Pia, sio lazima iwe mwaka mzima. Kila mwanafunzi wa sekondari anaweza akafanya hii kitu wakati wa likizo -- unafanya masaa fulani na unaandika ripoti ukimaliza.
Itapunguza Vijana vijiweni... na kuwafundisha kuwa wananchi wawajibikaji wenye kuweza kuleta mabadiliko.
what if national service - or an adjusted form of this service that is catered towards community development for example - is encorporated with secondary education (all 6 - 7 years of secondary learning)?
ReplyDeleteit's important to realize the benefits of some form of national service i think. while todays generations don't have to go through with it, i still see a more solid grounding in previous generations on Tanzanian history, culture, and solidarity.