Thursday, June 3, 2010

Unakumbuka enzi zile?

Kucheza gololi, matairi, magari ya makopo, cha ndimu (angaisha bwege, tobo bao na gombania goli), kutengeneza manati na kuwinda ndege, kudaka panzi, kidali po, kombolela... Bila kusahau kufuga samaki (nilikuwa na magapi kibwena! i.e. guppy aka Poecilia reticulata).


I got this film from Jadili Africa facebook page. Jadili Africa was founded in 2010 by conscious Africans who always dream of a peaceful Africa that is in peace with itself. I will encourage you to join the group if you want to see more short clips, articles, documentaries and news about Africa -- covering all sorts of angles; from politics to sports, cultures to myths, history to tourisms, shaky times to triumphs and many more.

8 comments:

 1. Sikujua kama jina la gapi nalo limetokea uzunguni. Mi nilikuwa na Siamizi Faita (Siamese Fighter), Zebra, Gold Fish sikuwahi kuwa nao (enzi hizo ilikuwa bei kinoma). Tukaenda baharini siku moja kutafuta mapango, habari zikamfikia bi mkubwa, tulikula stiki tulivyorudi, balaa, sikwenda tena baharini. TENAAAAA. (nina kweramu moja mpaka leo SN)

  ReplyDelete
 2. Hahahaha! Haukuwa na angel fish? Leopard? Mzee nilikuwa nabana hela za matumizi ya shule ili ninunue samaki. Maza alimaindi nilipoweka kweramu sebuleni - lilikuwa limejaa magapi watoto tu! Baadae nikafanikiwa kumpiga mzinga ili ninunue gold fish; maza baada ya kuwaona, dah! akawa ananipa hadi hela ya kununua uduvi (msosi wa samaki)!

  Kule kwetu Keko na Chang'ombe kulikuwa na wajanja sana. Ukiingia kichwa kichwa unaweza ukauziwa perege kutoka kwenye ile mifereji pale Kibasila. Baada ya siku kadhaa unashangaa tu "magapi" wako wanaanza kuota masharubu!! Akili kumkichwe. Gooood times.

  Vipi kuhusu kucheza cha ndimu? Unakutana na majeba wamekomaa ugoko kama tofali! Ngoja niishie hapa kwa sasa, maana'ke...

  ReplyDelete
 3. mixer, mkasi, kitambaa,glas...lol...wale wa rangi ya njano walikuwa wanaitwaje tena?..kuna mshkaji alikuwa anaitwa briton anakaa kimara...alikuwa na samaki balaa....hela yote ya tuition na nguo iliishia kwake..mhhh...

  ReplyDelete
 4. Du wazee mmenikumbusha mbali sana. Mie pia nilisevu kununua kwerium. Yaani samaki walikuwa wananikeep busy kichizi...gapizi, redi sota, kitenge, zebra, n.k na jamaa wengine kama alivyosema mdau hapo juu jamaa walikuwa wanatusakizia wenzao maperege, kuna jamaa alikuwa anawapata samaki pale Azania secondary kulikuwa na bwawa fulani, anatuingiza mjini sie watoto wa Upanga. Du, mambo ya uduvi sometimes nilikuwa natwanga dagaa mwenyewe home. Vipi yale mambo ya kwenda kutafuta majani ya samaki baharini kule ocean road/Agha Khan Hospital karibu na Ikulu (Dengu beach), mawe na shells. Pia kulikuwa na vitoi(plastic toys) fulania vya askari wa plastic unavitia kwenye kweramu kupendesesha. Kulikuwa kuna Rafiki yangu Fulani anaitwa Abraham Chuwa yeye kwerium yake ilikuwa safi sana, sijui oxygen gas nini!!!, kipindi icho mie sielewi chochote.
  Du nimekumbuka mabali sana.

  ReplyDelete
 5. Hahahaha @ Anon + Bata. Kumbe watu wengi mmepitia haya. Kuhusu haya mambo ya kuingizana mjini utotoni, yametupa maujanja. Na kuna stori za masela wangu nikisikia (wamekuwa matapeli) hata sishtuki!

  Ukiacha mikasa ya perege/magapi, kulikuwa na black fish. Nadhani mnamkumbuka huyu... Sasa kuna wale wajanja waliokuwa wanatafuta viluilui* kwenye madimbwi halafu wanawauzia wenzao (mpaka sh 500). Kituko ni pale dogo anapogundua "samaki" wake wanaanza kuota miguu na size ya vichwa inaongezeka; baada ya wiki kadhaa mikia inakatika! Nadhani unapata picha ya dogo anapogundua kuwa ameuziwa vyura. Kuna watu walikuwa makatili sana jamani..LOL

  *viluilui ni chura wachanga, ni weusi na wanafanana na 'black fish':

  http://sites.google.com/site/missgonzaleswebsite/_/rsrc/1239604557056/technology-enchanced-lesson-ii/cycle2.gif

  ReplyDelete
 6. umenikumbusha mbali sana nimependa hii sana uendelee kutuletea hizi habari za vijijini tunafaidi sana hasa sisi tulioko nje ya tz safi sana hii ni bora kuliko zile picha zinadhalilisha dada zetu tuletee kwa wingi kama hii ubarikiwe sana

  ReplyDelete
 7. Zawadi yako Anon (8:14 PM):

  http://vijanafm.blogspot.com/search/label/Lars

  ReplyDelete
 8. walahi yeyote aliyekulia Tz halafu hajawahi kuendesha ringi, "kujenga" manati, "kujenga" gari, kucheza mabento, visoda, msingi binua, kidali po, kombolela, kujificha, knasa panzi, kunasa ndege, tikiri, bao, rede/nage, kitenesi, gololi... anatakiwa akifika Mbinguni akiulizwa anachotaka duniani aseme kurudia utoto akacheze hii michezo. mwe! Asante sana SN kwa video hii. Hoooome sweet home! Ya kale dhahabu. Memories are made of these.

  ReplyDelete