Monday, June 7, 2010

UNAWE-Tanzania

Kuna baadhi ya mambo unayaona au kuyasikia na hukupa motisha ya aina fulani - hasa yanapotokea nyumbani. Kitu muhimu zaidi ambacho hukufanya hata uanze kujivunia ni watu wanaojitolea kuwafundisha wadogo zetu na kuwaandaa na dunia hii ambayo inaendelea kutekwa na sayansi ya teknolojia.

Mara nyingi nikitembelea tovuti ya UNAWE-Tanzania, nashindwa kujizuia kujiuliza maswali mengi. Ingekuwa vipi kama ningefundishwa na timu ya kaka Mponda? Je, kama ningeoneshwa mwezi, sayari nyingine, nyota na vimondo wakati bado niko mdogo, mambo yangekuwa tofauti? Kusema ukweli kuna wakati nawaonea donge watoto wanaopewa nafasi na UNAWE-Tanzania. Na nina uhakika juhudi zao zitazaa matunda ambayo yataleta mabadiliko kwenye jamii yetu kwa namna moja au nyingine.

Nakumbuka nilikuwa napenda sana masomo ya sayansi. Na nilijifunza jinsi ya kukokotoa maswali ya lenzi (i.e. ray optics), nilikariri majina ya sayari zote (na idadi ya miezi yao) na hata umbali wao kutoka kwenye jua. Lakini nilikuja kuiona telescope kwa mara ya kwanza nilipokuwa kidato cha pili! Nadhani unaelewa kwanini nawaonea donge wadogo zangu.

Wiki chache zilizopita, UNAWE-Tanzania walipokea vitabu, CDs na vifaa vingine muhimu vya kufundishia. Bahati mbaya au nzuri, kuna baadhi ya vitabu ambavyo itakuwa vema vikitafsiriwa kwenye lugha ya Kiswahili. Kwahiyo, wasiliana nao kama unaweza kuwasadia.

Nakusihi utembelee tovuti yao mara kwa mara ili kufuatilia vitu wanavyofanya. Kama hutaweza kuwasaidia kwenye mradi huu wa kutafsiri vitabu, nina uhakika hapo baadae unaweza ukawasaidia kwa njia nyingine.

Pongezi zangu ziwaendee UNAWE-Tanzania! Nitaendelea kuwatupia jicho kama kawaida yangu.

2 comments:

  1. Napenda Kuungana Mkono na SN katika kufanikisha ndoto za wadogo zetu. Kuna haja kubwa ya kutafsiri vitabu na material mengi ambayou UNAWE-Tanzania yanavyo mpaka sasa. Tumefanikiwa kuweza kuwafundisha Watoto katika lugha ya Kiswahili lakini kutafsiri material bado hivyo tunaomba mtu anaependa kushiriana nasi ajitokeze ili kuweza kuinua kiwango cha uelewa cha watoto wetu.

    ReplyDelete
  2. Natumaini baadhi wataitikia wito wako, Mponda. Nadhani huu ni mradi wa muda mrefu, au? -- kwasababu itakuwa vizuri kukiwa na kitu sustainable (in a long run).

    Binafsi, mambo yamebana sasa hivi. Lakini nikishuka pande hizo nitajaribu kukusaidia (nitawasiliana nawe kwa barua pepe).

    ReplyDelete