Sunday, June 13, 2010

Nelson R. Mandela - 46664

Picture: Nelson Mandela by Sue Dickinson

Filamu ifuatayo ni ya historia ya Nelson Rolihlahla Mandela, kwa maneno yake mwenyewe -- kwa kifupi. Angalia jinsi wazee wetu walivyotaabika, wakajitoa mhanga ili mimi na wewe leo tuweze kusimama bila uwoga na kutembea mitaani na vifua vyetu mbele.

Sijui unapata hisia za aina gani unapoona na kusikia hadithi kama hizi. Binafsi, napata motisha isiyo kifani na sichoki kuwashukuru wanaharakati kwa mambo waliyofanya. Leo hii naweza kuandika chochote ninachotaka kwenye blogs na vyombo vingine vya habari; sauti yangu inasikika. Sitetereki pale mtu anapoanza kunirushia maneno ya kibaguzi. Naamini kuwa sehemu kubwa ya mafanikio kwenye maisha yangu itatokana na juhudi zangu mwenyewe.

Bahati mbaya watu wengine wanatumia uhuru huu huu kujinufaisha wenyewe na familia zao; wamesahau machozi, jasho na damu ya wanaharakati kama Madiba. Wamewahi kujiuliza: Tungekuwa wapi kama watu na viongozi kama hawa wangeamua kupigana kwa ajili yao na familia zao tu?

4 comments:

  1. Wengi wetu tunajisahau na kupuuza mchango wa wapiganaji kama hawa. Hivi majuzi tu, watu wa South Africa walikuwa wanawachapa mapanga wananchi wa nchi nyingine za Africa. Zile Xenophobia attacks - yawezekana zilikuwa overhyped by the media, lakini ukweli upo - chuki ya ukabila bado ipo, sadly.

    ReplyDelete
  2. Sometimes huwa nawaza, whats the point kujitoa mhanga wakati watu hawatakuwa na shukrani wala nini...ila nikiangalia clips kama hizi zinanikumbusha umuhimu wake....

    Mimi nashukuru Mungu Nyerere alizaliwa Tanzania. Otherwise wakoloni wangekuwepo bado wapo nchini kwetu....Live long Nyerere..

    ReplyDelete
  3. I couldn't agree more with SN, Joji and Bata.
    May God bless Mandela. May God bless Nyerere. May God richly bless all the great people and leaders we have been blessed to have today and in the past days. I will never get enough of these people's wisdom. I have learned so much from listening and watching them. Each day I set myself to listen to them, I get a new thing. I may listen to the same tape over and over but each day that I happen to do so, I get a slight different meaning.

    May God richly bless these people and give them a special hearing in the judgment day. I really do not care the little mistakes they have made in their lives, I care about the people who might have been hurt by their decisions but I urge them to remember that we have never and we will probably never have a perfect human being. To human is to err. Those who point fingers they should as well remember that themselves have hurt people surrounding them.
    Thank you so much SN for this clip.
    I loved watching it and I learned a lot from it.

    ReplyDelete
  4. Bila shukrani.

    Hivi, mnadhani labda tuna watu wenye uwezo wa kuongoza, lakini kutokana na hali halisi wameamua kufanya mambo yao binafsi? Kwasababu watu hatuna shukrani? Au hatutatambua umuhimu wa vitu wanavyopigania?

    Ukiacha mambo ya uongozi, nadhani dhana hii hii ndio inapelekea watu kuonekana sio wazalendo; wasiokuwa na mapenzi na nchi zao. Utakuta mtu ana kazi yake nzuri, watoto wana uhakika wa kupata elimu nzuri -- lakini kuna vitu vya kumsukuma mtu kama huyu kuwa mzalendo? (Najua sio lazima uishi ulipozaliwa ili kupigania unachoamini... Lakini kuna baadhi ya mambo lazima uingie mitaani).

    ReplyDelete