Wednesday, June 9, 2010

Mbu na harufu ya pombe

Habari si njema kwa 'wanywaji' bongo. Utafiti umeonyesha kuwa, mbu wanaosababisha malaria wanavutiwa mno na harufu ya aliyekunywa bia. Mbu kama wadudu wengine wengi wana uwezo mkubwa wa kuhisia harufu mbalimbali - insect repellant nyingi zinatumia sifa hii ili kufukuza mbu. Katika utafiti huu uliofanyika huko Burkina Faso, watu 43 pamoja na mbu takribani 2500 walitumika ili kuweza kudadisi athari zozote kwa mbu zitokanazo na unjwaji wa bia.

Watafiti hawa wanaeleza kuwa metabolism ya bia mwilini inabadilisha kemikali fulani za harufu zitokazo ngozini na hivyo harufu itokayo baada ya kunywa bia yaweza kuwa inawavutia mbu hawa. Pia wanadokeza kuwa, baada ya bia kunywewa kinga mwilini hupungua, kwahiyo mbu kwa namna fulani wameweza kujenga uwezo wa kuhisia upungufu huu na hivyo kupendelea zaidi harufu ya waliokunywa pombe. Utafiti zaidi wahitajika ili kufahamu ni signatures gani za harufu zinazobadilika ambazo zinavutia mbu hawa. Itabidi tuanze kupiga 'tungi' ndani ya neti.


3 comments:

  1. Joji, jamaa wamezungumzia pombe za kienyeji (lubisi, ulanzi, gongo, chang'aa, pingu..)? Yaani ishu ni 'alcohol' au aina ya pombe pia inachangia?

    ReplyDelete
  2. Utafiti huu umefanyika kutumia pombe ya kienyeji iitwayo 'dolo' yenye alcohol content (~3%). Ninadhani aina tofauti ya pombe inabidi zitumiwe ili kuweza ku'replicate matokeo haya. Ila, hawajui ni nini hasa kwenye pombe (yaani content) kinachosababisha matokeo haya

    ReplyDelete
  3. Dah, mi' najaribu kuweka picha ya mtu aliyelewa halafu asikie hii habari? Nadhani stimu zote zitaisha!

    ReplyDelete