Monday, June 7, 2010

Mimi na blogs na facebook!

Na "Mtu Fulani"

Kama kawaida yangu, napata habari sahihi kutoka kwenye tovuti yangu ya Wavuti huku nikipiga mzigo. Nikipata upenyo natupia jicho blog ya Michuzi Jr kucheki ana picha gani asubuhi hii. Ni mwiko kuvunja utamaduni wa Mtanzania mwenye mtandao -- lazima nicheki mambo gani yanajiri kwa Michuzi aka Mzee wa Masafa ya Mbali. Ah! Hakuna atiko mpya ya Mashaka na inaonekana kama pamedoda kiasi fulani. Ninaperuzi kuelekea chini taratibu nikiangalia picha za matukio mbalimbali; nakutana na post ya salamu kutoka kwa Kamau!

Mhh! Kuna maoni zaidi ya 150?? Mashaka kabadili jina nini!? Nasoma ujumbe wa Kamau taratibu halafu najitosa kwenye maoni. Wabongo kumbe tuna hasira kiasi hiki? Wachafuzi wa hali ya hewa ni wengi, lakini kama wahenga walivyosema, penye wengi hapaharibiki neno. Naona baadhi ya maoni yenye mawazo mazuri. Lakini hizi nguvu zingepelekwa kwenye matatizo ya nchi zetu hizi mbili nadhani tungepiga hata hatua moja ndogo ya mtoto mdogo.

Baada ya kumaliza kazi zilizoko mbele yangu, naenda facebook kuona masela wanafanya nini na kutembelea kurasa za maselebriti wa Bongo. Namcheki msela wangu kutoka kitaani, Gillsant -- mshkaji hata akiweka nukta kwenye status yake, comments zinatiririka! Ana marafiki karibia buku tano... Kwahiyo wale wenye blogs zinazotafuta umaarufu hutumia ukuta wake kama ubao wa matangazo.

Namcheki Prof. Jay ambaye alipotea kidogo baada ya kuonekana kavaa uzi wa kijani. Kama kawaida yake anabadilishana mawazo na mashabiki wake. Inaonekana muda na ukimya vimepoza maswali yaliyokuwa kwenye vichwa vya wengi. Naenda kwenye ukurasa wa Fid Q kuangalia kama ameposti mistari na vina vipya. Jamaa mistari yake imeshiba; shule tosha na anaweza kukuambukiza uanaharakati kutokana na msimamo wake.

Ngoja ni-search kucheki kama Juma Nature naye yumo facebook. Kudadadadadeki, Nature ndani ya nyuuumba! Ana mashabiki 46 -- ngoja tucheki itamchukua muda gani kufika mashabiki 1000.

Dah! Nadhani inatosha, ngoja nirudi mzigoni. Lakini kabla ya ku-sign out lazima nipate ile kitu roho inapenda: Picha murua.

Nabofya sehemu fulani na naishia kwenye ukurasa wa Vijana FM. Dah, panatia huruma kwasababu pamedoda ile kinoma. Labda wakiweka picha nzuri za watu maarufu watapata mashabiki zaidi (angalau wafike 500 tu).

Nachoropoka kutoka Vijana FM na kuishia kwenye ukurasa wa Ray C. Naperuzi picha zake haraka haraka kwasababu nimeshaziona nyingi.

Vitu vitamu havihitaji haraka kwahiyo natembelea ukurasa wa K-Lynn mwishoni kabisa. Mke wa mtu hasifiwi, lakini nimeamini kuwa Wabongo ni wabishi!

Na-sign out na kutupia jicho blog ya Mange. Duh, nilidhani blog bado ni changa lakini inapata hits zaidi ya buku tano kwa siku! Kwa mwendo huu, hii nd'o itakuwa mama ya blogs zote Bongo. Michuzi itabidi akae chonjo.

Ngoja nirudi mzigoni.

9 comments:

  1. Tatizo je zinamanufaa kwa jamii au ndo basi tu?

    ReplyDelete
  2. Mtu fulani, kula 5 rafiki. Yaani nimejiuliza hii posti imefikaje mwisho? aa safi sana VijanaFM, mnakuja juu kwa kasi ya ajabu walahi lazima hits hapa zianze kugonga 1000 kwa siku na ndani ya mwezi wa nane tuanze kuzungumzia 5000 hivi. Saafi sana vijana wa VijanaFM, huu ndiyo mwendo, burudani, elimu, ubunifu, hapa na pale, saaafi sana! Mi napenda sana hii, nafurahia, najifunza. Kula tano VijanaFM.

    ReplyDelete
  3. Subi, hits 1000? Hatutafika uko nadhani. Ni kujaribu kupeana taarifa tu za hapa na pale na kujaribu kuwa tofauti kidogo.

    Shukrani kwa kuwa viewer nguli wa Vijana FM!

    ReplyDelete
  4. Subi, I wish your prediction were true, sadly it is not. Most Tanzanians with access to the internet will not fancy this blog due to its somehow "intellectual-ness". People seem to prefer gossip and such therefore it is not suprising that those blogs which supply such will have more visitors.

    Medusa

    ReplyDelete
  5. True, I don't think we will ever reach those figures. I am just happy with Vijana FM's gradual growth.

    Kama mna maoni, michango n.k. msisite kutudokeza.

    ReplyDelete
  6. What's with all the pessimism SN?

    ReplyDelete
  7. Just being realistic, man.

    ReplyDelete
  8. Vijanafm is still young. Ila, tukiji'limit na kusema kuwa hatuwezi kufikia hits za juu ninadhani tutakuwa just another random blog. Who says gossip news should forever capture the attention of TZ peeps? Keep up the good job guys and one day this space will be the talk of the town. Vijanafm aim high.

    ReplyDelete