Nadhani watu wengi watakuwa wamesikia au kuona hali kwenye vyuo vikuu au vyuo vya elimu ya juu kwenye miji mbalimbali kwa njia moja au nyingine, iwe Ulaya, Afrika, Amerika au Asia. Na Vijana wengi zaidi wanatamani au wana mipango ya kusoma nje ya nchi.
Bahati mbaya upatikanaji wa 'info' muhimu kwa Vijana ambao wanataka kusoma nje sio rahisi sana kama inavyopaswa kuwa, hasa Tanzania. Sijui hii inatokana na nini haswa; kasumba ya vizazi vilivyopita? Uchoyo wa Vijana ambao wako nje tayari? Uwoga?
Hilo sio dhumuni la nakaka hii. Lakini watu waliopata nafasi ya kusoma nje watakuwa wameshuhudia ufinyu wa Vijana kutoka Tanzania - ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika - kwenye vyuo mbalimbali hasa Ulaya. Kuna sababu nyingi zinazochangia hili, lakini kwa mtazamo wangu nadhani labda hali inaanza kubabadilika kadri miaka inavyoenda.
Dhumuni la nakala hii ni kujaribu kuwapa Vijana na wazazi picha ya hali halisi kwenye vyuo vilivyopo kwenye miji mbalimbali duniani. Kwahiyo nawaomba wale ambao wanaosoma na waliosoma kwenye vyuo vya nje kuwapa picha halisi (ya kuwa wanafunzi kwenye nchi za watu) Vijana wenye ndoto za kufuata nyayo zao.
Unaweza kutoa rai yako kwa njia yoyote unayokufaa. Kama unakwazwa kidogo unaweza kutumia mfumo ufuatao, ukijibu maswali mbalimbali:
______________________________________________________________
- Chuo ulichosoma, mji, nchi [website]
- Ulisomea/Unasomea nini? Ukubwa wa 'department'.
- 'Info' muhimu kuhusu scholarships/grants/financial aid/loans.
- Vipi kuhusu 'social life', matatizo ya lugha, ubaguzi, upatikanaji wa misaada pale unapokumbwa na matatizo. Kuna urahisi wowote kwa ajili ya maisha ya mwanafunzi?
- Na vitu vingine ambavyo unadhani ni muhimu, kwa mfano upatikanaji wa 'student jobs' n.k.
______________________________________________________________
Maswali yanakaribishwa pia. Ukumbi ni wenu Vijana! Mnakaribishwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Watanzania tulichelewa, ila sasa ninadhani tunakuja juu. Kuna maelfu wa vijana wa kitanzania katika bara la Asia - Malaysia, India, Urusi, China, na wengine wengi katika Ulaya mashariki Ukraine, Uturuki, Poland n.k Kwahiyo katika pande za huko nadhani tumetia fora, wanaosoma huko watupe data.
ReplyDeleteIla ukija katika 'modern popular' places kama US, UK, Germany, Holland wanafunzi wa TZ ni wachache mno kulingana na mataifa ya Kiafrika mengine.
Miaka ya nyuma tatizo kubwa lilikuwa ukosekanaji wa taarifa. Ofkoz, kuna ile kasumba ya kutokuwa na motisha ya kushughulikia process (kuchangamkia tenda, act) - initiative. Huwa ninaishiwa nguvu nikipata email mtu ananiomba nimtafutie chuo. Mtu mwenyewe anayesema hayo ni graduate wa chuo kikuu TZ, na haishi kijijini. Anyway, sahivi kuna kundi la vijana ambao wamejikita kusaidia wenzao kwa kutoa taarifa muhimu kuhusu nafasi za scholarship, pamoja na application process:
http://people.trentu.ca/peternalitolela/universities.html
http://makulilo.blogspot.com/
This comment has been removed by the author.
ReplyDeleteShukrani kwa kufungua dimba na kutupa websites ambazo zimekuwa zikiwapa watu wengi info muhimu hasa zinazohusu application process! Mtu anapokuja kukwambia, "Nitafutie shule na scholarship," akili huchoka hata kabla ya kuanza kufikiria uanzie wapi.
ReplyDeleteNitajaribu kutafuta watu wengi kadri ninavyoweza ili waje watupe mchango wao. Na mimi pia nikipata muda nitaelezea 'vichochoro' nilivyopitia kwa kirefu.
Ndugu zangu mliopo Uholanzi (TU Delf, Eindhoven, Amsterdam, Twente), Ubelgiji (Gent), Ujerumani (Jacobs University Bremen, Munich, Hamburg, Muenster, Essen),UK (Leeds, Manchester), Poland, Estonia, Urusi, India (Delhi, Bangalore), Sweden (KTH), Thailand, Malaysia, Singapore...n.k. nategemea michango yenu.
Hizi process za kutafuta chuo nchi za nje, hasa hasa nchi zilizoendelea za magharibi inahitaji moyo na kujipanga mapema. Mchakato mzima si lelemama, kwani ukitaka kulipiwa au kusoma kwa scholarship ni muhimu uifanyie kazi ‘application‘ yako.
ReplyDeleteNitaodhoresha hapa chini mchakato kwa jinsi nilivyopitia mimi (vyuo vya ulaya). Nitawapa timeline na kuelezea ni yepi niliyafana lini. Maelezo nitoayo hapa ni experience yangu tu, na sisemi kuwa nilichofanya mimi ndio njia pekee ya kuandaa application yako. Ni kukupa mwangaza tu.
Septemba – Oktoba ya mwaka kabla ya masomo kuanza.
Jambo muhimu ni kujitayarisha mapema. Ninamaanisha jipe mwaka mmoja kwa ajili ya kuanza process mpaka muda ambao unategemea kuanza program yako. Kama upo B.Sc, anza angalau kuperuzi na kukusanya info kuhusu masters unapoanza mwaka wako wa mwisho wa masomo: program nyingi Ulaya zinaanza Septemba, kwahiyo anza kukusanya info angalu miezi kumi kabla ya tarehe hii.
Ukishakuwa na uhakika kuwa unataka kufanya masters, jikite sasa kutafuta chuo ambacho unadhani utaweza kunufaika katika masomo yako. Je, aina ya tafiti (research) zinazofanywa katika vyuo vinavyokuvutia?
1. Kusanya listi ya vyuo mbali mbali uonavyo na kuviita ‚target schools‘. Waweza kupata listi ya vyuo mbali mbali kwenye tovuti kama:
http://www.timeshighereducation.co.uk/hybrid.asp?typeCode=431&pubCode=1&navcode=148
Binafsi niliitumia hii kwa kutazama vyuo vinavyoongoza katika sekta na tafiti nizipendazo mimi binafsi.
2. Baada ya kuwa na listi ya vyuo kama 15 hivi (vilivyopo Sweden, Uswisi, Ujerumani, Uingereza, Ubelgiji, na Uholanzi) ambavyo ninadhani vinafanya tafiti nipendazo mimi nikaanza kuchambua chuo kimoja kimoja na kufupisha listi kwa kutumia vipengele zaidi. La muhimu hasa ni uwepo wa scholarship. Baada ya hapo nikawa na vyuo kama 6 hivi. Kati ya hivi nilikuwa na chuo kimoja ambacho kuchaguliwa ni mbinde, na 4 ambavyo nilidhani ninanafasi nzuri ya kuchaguliwa na kimoja kama safety. Vyuo vyote hivyo kwa namna moja au nyingine vilikuwa na aina mbali mbali ya misaada kifedha (financial aid) – stipend, tuition fee scholarship, ama mkopo.
Kupata listi hii ndogo ilinichukua kama wiki 2-3 hivi.
3. Baada ya hapo nikatia kichwani tarehe ya mwisho ya kutuma makabrasha ya maombi (application deadline) kwa kila chuo (Sweden ni January kati, Uswisi ni December 1 au Aprili 1 – inategemea na chuo, Ujerumani ni Aprili).
ReplyDelete4. Vyuo vyote vilihitaji barua (recommendation letter) ya wakufunzi angalau wawili. Muda huu nikawataarifu ma’Prof nia yangu ya kutuma maombi ya masters vyuo vya Ulaya. Wahadhiri niliowasiliana nao ni ambao wananifahamu vizuri kutokana na kazi za darasa, maabara na hata ‘socially’. Nikaomba ushauri wao pia kuhusiana vyuo ambavyo wanadhani vipo ‘juu’ katika tafiti fulani fulani.
November - December ya mwaka kabla ya masomo kuanza.
Katika kipindi hichi nilianza kutayarisha ‘research proposal’ ambayo ningeiambatanisha kwenye ‘statement of purpose’ au ‘letter of motivation’ iliyohitajika katika maombi.
Katika hiyo barua nilijaribu kuainisha ni kwanini wanichukue mimi hasa (nilielezea kiundani ‘background’ yangu katika field/internship, tafiti binafsi, tafiti za chuo nk). Jaribu kuzingatia nafasi ya maandishi wanayokupa, kama wanasema barua yako isizidi maneno 500 usizidishe! Na kama hawajaainisha, usijaribu kuandika kitabu. Epuka copy and paste katika barua hizi, kwani kila chuo ni tofauti na hata kama tafiti zifanywazwo katika vyuo utakavyo’apply mara nyingi wanapenda kusoma ‘specific details’ na sio vitu vya kiujumla kuhusu wao.
mfano wa mtiririko wa ‘letter of intent’:
aya ya 1: eleza kiujumla ni aina gani ya tafiti au masomo yanayokuvutia wewe kiufupi.
aya ya 2/3: fafanua na eleza kimuhtasari kazi ulizowahi kufanya (katika tafiti, au miradi) – ongelea zinazohusu masomo yako (Mimi nilibeba mabox ila sikuandika hayo ). Ni nini ulijifunza, ulitumia nyenzo gani, na ulinufaika kivipi?
aya nyingine: fafanua ni kwanini unadhani unataka M.Sc katika sekta hiyo?
aya nyingine: eleza ni kwanini unataka kujiunga na chuo husika, na ni mhadhiri/kundi gani unataka lisimamie tafiti zako. Je, utanufaikaje ukisoma katika chuo hicho kuzidi vyuo vingine kama vya awali uliposomea.
Mtiririko huo ni kukupatia mwangaza tu, hii sio dogma. Wapatie watu wengine wenye kufahamu kiingereza safi waisome na wakupe feedback.
Baada ya kuwa na maandishi kuhusu ni nini hasa ninachotaka kunufaika katika masters, nikawasiliana na wakufunzi walioniahidi kuniandikia recommendation. Niliwaambatanishia barua yangu hiyo ili wapate undani ni kipi kinanivutia katika kila chuo, niliunganisha pia CV yangu, transcript, pamoja na anuani ya vyuo ninavyo apply.
ReplyDeleteMitihani ya ziada
Binafsi sikuhitaji kufanya mitihani ya ziada kama GRE au TOEFL, ila fahamu hili mapema kwani kujiandikisha kwa mitihani hii inachukua muda na ni ghali.
Matayarisho mazuri pia ni kuwa na kozi ambazo zinakupa mwanzo mzuri wa kuendelea na masomo yako. Ukiwa umefanya kozi za neuroscience tu katika bachela na unaomba masters ya microbiology, itakuwa ngumu kidogo.
Januari
Katika kipindi hiki nilituma makabrasha yote katika vyuo vyote nilivyotaka kujiunga navyo. Nusu ya vyuo hivyo deadline yake ilikuwa miezi kama miwili baadaye.
Mtiririko huu ulinisaidia kuchaguliwa katika vyuo vyote nilivyotuma maombi. Kutokana na ufinyu wa nafasi siwezi andika yote hapa ila ninadhani umepata mwangaza.
Kwahiyo ujumbe wangu wa vijana wa Tanzania ni kwamba jipange na fahamu mapema nia yako.
Sahivi nipo hapa ( http://en.wikipedia.org/wiki/ETH_Zurich ) nikifanya M.Sc yangu.
Ukitaka kufahamu zaidi procedure za kuapply hapa tembelea:
http://www.ethz.ch/prospectives/admission/index_EN
Kuna financial aid program kadhaa hapa chuoni, tembelea:
http://www.rektorat.ethz.ch/students/finance/scholarship/excellence/index_EN
http://www.sbf.admin.ch/htm/themen/bildung/stipendien/eskas_laender/Tansania_en.html
Ukitaka kuja uswisi, hasa hasa wale wanaohusika na field za teknolojia na uhandisi tembelea pia tovuti ya chuo cha EPFL:
http://futuretudiant.epfl.ch/page12313-en.html
kuhusu social life na maswali mingine nitaandika baadaye.
Ni hayo tu kwa sasa vijana wenzangu.
Enzi za kujaziwa application form zimeisha, tujitume.
Joji, shukrani mzee. Mchango wako unahitaji thread tofauti! Mimi ngoja nitoe mchango wangu kwa kuanzia na bachelor's degree kwenye chuo nilichopitia.
ReplyDelete_____________________
Jacobs University Bremen, Germany [www.jacobs-university.de]
Jacobs ni chuo 'private' chenye wanafunzi zaidi ya 1500 kutoka mataifa zaidi ya 80. Application na admission process inarandana na ile ya vyuo vya Marekani na lugha inayotumiwa ni Kiingereza. (Lakini ni jambo la busara kujua Kijerumani kidogo, angalau cha kuulizia njia, msosi na namba za simu :)!)
Bahati nzuri Jacobs wanatoa aina mbalimbali za financial aid - scholarships, grants na loans. Na mara nyingi ukishapata admission, financial aid package inafuata kutegemea na hali yako (na matokeo ya shule ya sekondari), ambayo hufanya maisha yawe rahisi...Sio lazima kubeba box!
Kusema ukweli hata mimi nilikuwa nina dukuduku langu kuhusu kusoma Ujerumani, hasa linapokuja suala la ubaguzi. Ubaguzi upo kila sehemu unayoenda (duniani) lakini ukiwa kwenye mazingira ya shule mambo ni poa kabisa; na hakuna mtu atakayekuzuia kusoma kwasababu wewe unatoka Tanzania.
Kwa bahati mbaya au nzuri undergrads wote wanatakiwa waishi kwenye campus, kwahiyo muda mwingi unakutana na watu/wanafunzi wenzako.
Mji wa Bremen ni mdogo, na maisha ni cheap sana kulinganisha na sehemu nyingine Ujerumani. Kama wewe ni mtu wa kula raha jiji la Hamburg liko jirani tu.
Maelezo zaidi yanapatikana kwenye website ya chuo.
We acha tu. Wahenga wanasema "Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza". Ila hayo tuyaache. Mi naona kama hao watu wanawauliza nyie wasaidieni tu. At least hao wanauliza. Wengine hata hawaulizi.
ReplyDeleteMimi nilisoma ( TU Delft & Jacobs University). Watanzania wengi niliokutana nao ni wale wenye "exposure" + TA (Teaching Assistants pale Mlimani). And in most cases embassies za nchi mbalimbali huwa wanakuwa na scholarship za MSc/PhD ( even BSc) alocated kwa watanzania. So watu huwa wanajaza form na kuchaguliwa na vyuo kadhaa( i.e DAAD(germany), NFP fellow(holland)...)
Ila kuna vyuo vingine vinakuwa na scholarship ambazo hata embassy hawajui. Hapo ndipo tofauti ipo. They expect you to apply directly. Sasa hapo ndio watu wengi hudhani labda hizi scholarship watu wanazificha au wanageana. Ndio maana mtu anakuja na kauli ya nitafutie mchongo wa scholarship.
Ukimpa website na info kama hizo anasema wewe unajua watu wengi huko labda utakuwa na influence. Huku hamna mambo ya kujuana. Tuma application tutaongea.
-----------------------------------------------
Delft University of Technology
TU Delft ni chuo cha zaidi ya miaka 100. Application process ni kama hiyo ilivyoelezwa na joji99 na Steven katika post ya juu yangu. Sio programme zote za BSc zinatumia english. Ila from MSc na PhD zote ni english.
Upande wa scholarship zipo. Ila hizi scholarship inabidi ufanye application mapema. Kuna Faculty scholarship, general scholaship, Shell Scholarships, NFP...etc. Ukiangalia website ya faculty unayoapply kutakuwa na kila information.
You also have to be persitent. Make sure all the forms have been filled and have arrived. Other than that, wadachi wako very friendly. You also dont need dutch since everybody speaks english here.
Maelezo zaidi yanapatikana kwenye website ya chuo www.tudelf.nl
------------------------------------------------
I'm not sure if my post is clear enough. Dont hesitate to ask me questions.
kiukweli nimefurahi sana na maelezo yaliyotoloewa hapo juu kuhusu application. but, naona wengi ni wale wa upande wa Science, I have not heard from those of Business schools, etc.
ReplyDelete