Tuesday, May 18, 2010

Propaganda za Fid Q zipo kwenye mtandao!!!

Haya jamani, wale ambao tulikuwa tunalalamika kuwa kupata CDs kutoka Bongo ni mbinde...


Album ya mzee mzima Fid Q, Propaganda inapatikana hapa (bofya)! Unaweza ukapata wimbo wake mpya Ngosha the Swagga Don hapa. Wimbo ni bombaaaaaa!

"Mc'z wanaenda down, ka Zim dollerz
mie sio mtu wa Bling mie ni Culture ka Zemkala
da brightest thang shinin nxt to a Diamond
niite Ghost writter ninapoBLAZE ka Amo
mara nyingi mie nina bahati kama Lotto Machines
sio mtu wa Adventures kama FRODO kwenye Lord of the Rings
niite ROSCOE, ninapoSPEAK in tonguez ka Jenk...inz
Don kama Bosco Mad kama Ice Helsink
unataka Bed fight? mie nina King size na French fries kwa Breakfast
T bone steakz na Prison break ki GANGSTA
Tatoo Plan kama Michael Scholfield
Bruce Lee wa RAP ya AFRIKA, ROCKCITY naigeza RAP SEAT...


"Alipenda kwenda na TAREHE, amesahau SIKU Hazilingani
PESA huja na STAREHE, na MATATIZO humo humo Ndani
Hakuna kinachokauka Mapema zaidi ya MACHOZI
japo MACHO hupaki Mekundu na USONI ishara ya Majonzi
Kizuri ni KIZURI lakini chenye UBORA Ni BORA
Kwa bahati MBAYA au NZURI akaja mchimba MADINI wa Kakora
Akashoboka n...a huyu BINTI Aliyemsafisha macho
Akamhonga, Gari, Nyumba na kile alichokuwa Nacho
Almesahau alitoa, MACHOZI, DAMU na JASHO,
kipindi ana HUSTLE, siku zi nyingi anaamini atarudi apoapo
Siku zote ADAM hakosi EVE wa Kumshawishi
Haijalishi maji ni ya MOTO lazima yataurudia UBARIDI..."

Mistari kama hii haina budi kununuliwa!

Monday, May 17, 2010

Leadership = knowing what, how, and why

More from SriBuo



Artist: Mimi Divalish
Album: Music In Me (album review here)

Download free album samples:
Mimi Divalish feat. Tinny: "Fa ma mi"
Mimi Divalish feat. Jane, Caroline, Dela, Sita, Pappi 5five: "Leave me alone (remix)"

Buy album:
- on iTunes
- on Amazon

Album art:
- SriBuo Media





Artist: Mzbel
Album: Saucy Girl (album review here)

Download free album samples:
Mzbel feat. Quata: "Sexy thing"
Mzbel feat. Shilo: "Odo kiss me"

Buy album:
- on iTunes
- on Amazon

Album art:
- SriBuo Media





Artist: Obrafour
Album: Asem Sebe (album review here)

Download free album samples:
Obrafour: "Odo"
Obrafour: "Enye nyame a"
Obrafour: "Bra be whe"

Buy album:
- on iTunes
- on Amazon

Album art:
- SriBuo Media

Sunday, May 16, 2010

May 20: Open Space Workshop in Dar

We recently came across this invitation on LinkedIn about an Open Space Workshop on youth and entrepreneurship, which is happening in Dar on May 20.

Details:
  • Title: Open Space Workshop on the future of Youth Entrepreneurship Development in Tanzania
  • Time: Thurs May 20, 2010, 8:00pm - Fri May 21, 2010, 3.30pm
  • Venue: Benjamin Mkapa Pension Towers, Serengeti Room, 2nd floor, Maktaba Street, Dar es Salaam, Tanzania (see map below)


Brief Description:
According to the open invitation, the focus question of the workshop is: “How do we unleash the energy and ideas of Tanzanian youth and start an entrepreneurship wave in Africa that will change the way we see self-employment and create employment opportunities for generations to come?”.

The even is organized by "the Youth Entrepreneurship Facility (YEF), a partnership between the Africa Commission, the Youth Employment Network and the International Labour Organization to Unleash African Entrepreneurship".

They mention on their invitation that they "hope to challenge the East African youth to create employment opportunities for themselves and for their peers and together with national partners we will support them in their efforts."

The conference is "based on the innovative and widely praised 'Open Space' methodology in which participants set the agenda and lead discussions around issues that they feel are crucial for the topic at hand."

Further details:
What is LinkedIn, and how do I get on it?
LinkedIn Open Invitation
About the Africa Commission
About the Youth Employment Network (and the youth-to-youth fund)
About the International Labor Organization

Saturday, May 15, 2010

Did You Know? 3.0

Some interesting data on education, technology, and society.

Outliers: the Story of Success


Hivi punde tu nimemaliza kukisoma kitabu cha Malcolm Gladwell kiitwacho Outliers: the story of success. Nimeona ni vyema kuwasilisha hapa machache kuhusu kitabu hiki ili nawe ukinunue na kukisoma. Kabla sijaendelea, ningependa kuweka bayana kuwa kitabu hiki sio 'self help book' - yaani vile tabu vinavyotoa listi ya ni yepi ya kufanya ili ufanikiwe kimaisha.

Katika makala iliyopita, SN alitupatia maswali na hoja muhimu kuhusu suala la motisha na mafanikio kiujumla kimaisha. Ndani ya Outliers, Gladwell anatupatia mwanga kuhusu sifa zinazowaunganisha watu kadhaa wenye 'mafanikio' katika nyanja mbali mbali. Anaeleza kuwa 'mafanikio' hayatokani na kipaji pekee yaani talent au genius, bali ni mjumuiko wa sifa ambazo mara nyingi hatuzifikirii kama bahati, malezi, mila, historia ya familia/uzawa n.k. Ni muhimu pia kuweka bayana kuwa hapa haongelei ile bahati kama ya kushinda bahati nasibu, bali aina ya bahati ya kuwa 'at the right place at the right time' na kuwa na uwezo wa kuitumia nafasi hiyo kwa manufaa yako kiufanisi.

Malcolm Gladwell ana kipaji cha kuchambua tafiti mbalimbali za sociology na kuzielezea kwa ufanisi kwa mtu wa kawaida (layman). Kwenye Outliers, anaelezea thesis yake kwa kutumia mifano ya maisha ya akina Bill Gates, Mozart, kundi maarufu la muziki the Beatles n.k. Anatuelezea kuwa Gates, ukiachilia mbali uwezo wake kielimu, mafanikio yake katika software industry yalitokana na kuwa na 'bahati' ya kusoma katika shule ya sekondari iliyokuwa na computer maalum isiyotumia punch-cards (pekee nchini US kwa wakati huo) iliyomwezesha kufanya mazoezi kwenye fani hiyo kuzidi wenzake. Nafasi hii na nyinginezo zilimwezesha ku'accumulate zaidi ya masaa 10,000 ya programming kabla hata hajaanza chuo, na hivyo kumfanya awe mtaalam kwenye fani. Anatueleza pia kwamba wale Beatles, chimbuko la umahiri wao katika muziki ulianza tu baada ya kupata 'bahati' ya kualikwa mara kwa mara jijini Hamburg kwenye shoo ndogo-ndogo zisizofahamika, na hivyo kuweza ku'accumulate masaa yao 10,000 ya mazoezi kabla hata ya kuanza kutumbuiza katika shoo kubwa.

Ndani ya Outliers, Gladwell anaeleza mifano ya umuhimu wa uzawa katika mafanikio, anatoa maelezo kwanini wayahudi wengi wanaendesha uchumi wa miji kama New York. Ohh, na pia hujawahi kujiuliza kwanini Wachina/Wakorea/Wajapani wengi ni wakali katika hisabati? Hasa hasa Wachina tunaokumbana nao vyuoni huku ulaya na marekani? Gladwell anaelezea kuwa chimbuko ni kutokana na lugha zao kuwapa advantage fulani katika kuhesabu, yaani zipo very concise kuzidi lugha kama kiingereza au nyingine nyingi. Sijui kiswahili kikoje katika fikra hii, ila hii ni mada nyingine ukizingatia kuwa nchini TZ hisabati bado ni gonjwa sugu.

mwandishi Malcolm Gladwell

Kitabu hiki kinachochea fikra, na ni aina ya vitabu ambavyo kijana wapaswa kusoma. Binafsi nimevutiwa na insights hizo mbalimbali, ingawa katika baadhi ya 'stori' kunakuwa na oversimplification fulani katika kutafuta chanzo - masuala ya causality na correlation. Ila utaweza kupata mwanga kuhusu ni yepi yanawafanya baadhi ya watu kuwa wa pekee. Are YOU an outlier? Je, tayari umeshakusanya masaa 10,000 katika fani uliyopo sasa?



Waweza kukinunua Outliers hapa: http://www.amazon.com/dp/0316017922
Soma kazi zake nyingine hapa: http://www.gladwell.com/

Thursday, May 13, 2010

Kufundisha Viongozi

Msomaji, nadhani wewe ni mmoja wa watu ambao wamebahatika kupata elimu. Je, unadhani unaitumia elimu yako na ujuzi wako ipasavyo? Matatizo unayoyaona kwenye jamii inayokuzunguka yanakugusa kwa namna moja au nyingine?

Mwezi uliopita niliandika makala kuhusu viongozi ambayo ilikuwa imeegemea kwenye siasa zaidi. Lakini leo ninakuomba uangalie video ifuatayo ya Patrick Awuah, kutoka Ghana, kuhusu viongozi kwenye nyanja nyingine muhimu kwenye jamii. Patrick anazungumzia fikra na mawazo yetu; umuhimu wa kuwa na fikra za majukumu ya kijana kwenye jamii. Kama wahenga wetu walivyosema 'samaki mkunje angali mbichi', Patrick anaongelea jinsi ya kuandaa watu kuwa Viongozi -- kuwafundisha na kuwafinyanya ili fikra zao ziweze kuwa na mawazo ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye jamii.

Tafadhali, ukipata muda msikilize Bw. Awuah kwa makini: