Tuesday, May 25, 2010

Tanzania ni Nchi ya Wapole

Mzazi: We Sikuzani, embu acha hiyo!

Mtoto: Kwanini!?

Mzazi: Kwasababu nimesema!

Haya ndio yaweza kuwa majibizano mafupi katika familia nyingi tulizokulia. Mtoto hapewi nafasi ya kujibiwa swali lake, na mara nyingi majibu yatolewayo ni ya ukali au ya kuonyesha utawala. Mara nyingine ukiuliza 'kwanini', unaweza kubalazwa kofi, kwasababu tu umemjibu mzazi!

Nimeamua kugusia mada hii muhimu ya malezi baada ya kusoma kitabu cha Annette Lareau kiitwacho Unequal Childhoods: Class, Race, and Family Life. Kitabu hiki kinatoa mwanga kuhusu tofauti za malezi zilizopo kati ya familia zenye kipato kikubwa/kawaida (mtaani tutaziita za 'geti kali') na zile za kipato cha chini ('uswazi'), yaani middle-class vs. working-class parenting. Muandishi amejaribu pia kueleza ni sifa gani zinawasaidia au kuwaathiri ukubwani watoto kutokana na tofauti ya malezi kati ya matabaka haya mawili. Ingawa tafiti ya kitabu hiki inahusu familia za marekani, kwa kiasi fulani mengi tunaweza kujifunza kuhusu mazingira ya malezi tuliyonayo Tanzania na jinsi gani tunajenga taifa potofu la wapole.


Lareau anaanza kwa kueleza tofauti mbili za malezi: malezi aina ya concerted cultivation (yanayofuatwa na wale wa 'geti kali') na ya accomplishment of natural growth (yanayofuatwa na wa kipato cha chini). Tofauti kati ya aina hizi ya malezi nitaziainisha hivi punde.

Ili kufahamu tofauti zilizopo katika aina hizi ya malezi, Lareau alifanya mahojiano na wanafunzi zaidi ya 80 wa darasa la tatu na nne kutoka familia za wamarekani weusi pamoja na wazungu. Katika kipindi cha utafiti wake, aliweza kubainisha kuwa aina ya malezi ya watoto inategemea na kipato (tabaka) cha (la) familia, wakati kabila (race) ya familia haina uhusiano wowote.

Kwenye malezi ya concerted cultivation aligundua kuwa, wazazi hawa wengi ni wa kisomo cha juu. Wazazi hawa wanahusika mno katika malezi ya watoto wao nyumbani na kwa kiasi kikubwa pia katika shughuli zao nje ya nyumba (kama ufuatiliaji wa maendeleo yao ndani na nje ya darasa). Wazazi wanashughulikia kuwatafutia na kuwaandikisha wanao katika shughuli za nje ya darasa zinazohitaji usimamizi wa wakubwa, mfano: uskauti, mafunzo ya kuogelea, mafunzo ya kupiga kinanda, n.k. Nia yao ikiwa kuwasaidia watoto wao wawe all-rounded ili kupata ujuzi zitakazowasaidia katika maisha ya ukubwani – hasa hasa katika kazi za utaalamu (white collar jobs). Pia, wazazi hawa mara nyingi walikuwa tayari kuingilia kati pindi kukitokea tatizo shuleni kuhusu watoto wao, pamoja na kukutana na walimu wa shule kuulizia maendeleo yao.

Pamoja na hayo, mazingira ya wanayokulia watoto hawa nyumbani ni tofauti (sio kifedha, bali kijamii). Laureau, anaeleza kuwa wazazi katika familia hizi wanajihusisha zaidi kuongea na wanao, na hivyo kuwasaidia watoto kukuza vocabulary au hata ari yao kujiamini. Ari hii ya kujiamini, inakuzwa kwani wazazi pia wanawahimiza wanao kuuliza maswali au ku’negotiate na wakubwa ipasavyo. Pia, amri zinazotoka kwa wazazi huwa zinaambatanishwa na maelezo ya kwanini wanatoa amri hizo. Hivyo, watoto hawa wanakuwa na mazoea mapema ya kuongea na wakubwa na kujua namna ya kujieleza (mf. matumizi ya eye contact), na hata kuwa na uwezo wa kujieleza mbele ya umati. Kumbuka watoto waliofuatiliwa ni wa umri wa miaka kati ya 7 na 9. Laureau anaeleza kuwa, 'ubaya' wa malezi haya ulionekana kwa ukithiri wa watoto kulalamika-lalamika ovyo, kutaka kuwa centre of attention, kuwa wabishi/watundu, kimbelembele, kutojua umuhimu wa pesa, pamoja na kutokuwa karibu na ndugu/koo.

Wazazi wa familia zenye kipato cha chini walifuata aina ya malezi ya accomplishment of natural growth. Katika malezi haya, mzazi hajihusishi mno katika dunia ya mtoto zaidi ya kutoa chakula, malazi, elimu, na mavazi. Tumaini la wengi wa wazazi hawa ni kwamba mtoto atakuwa (atapevuka) tu, sponteaneously – yaani, 'muache mtoto awe mtoto'. Lareau anaandika kuwa, watoto wa malezi haya muda wao mwingi baada ya shule hutumia kucheza na wenzao na hawana ratiba iliyobana ya extracurricular activities kama waliokuwa nayo wa 'geti kali'. Katika malezi haya mazingira au ‘dunia’ ya nyumbani ya mtoto na mzazi ina mipaka thabiti. Mzazi hajihusishi kwa kiasi kikubwa na kazi za mtoto za nyumbani, na mara nyingi wazazi wanatoa amri/adhabu kwa wanao bila hata kumueleza mtoto ‘kwanini’ (mf. Sikuzani na mzazi). Hivyo, watoto wanakuwa na woga kujieleza kwa mamlaka (watu wazima), na mara nyingi wanakuwa na heshima binafsi ndogo (self-esteem). Uzuri wa malezi haya yanafahamika na wengi, kwani katika jamii ya nchi yetu ni aina hii ya malezi inafatwa. Sifa chanya ni kama watoto wanakuja kuwa wakarimu/diplomatic, waangalifu katika masuala ya pesa, n.k.

Lareau anaonya kuwa, hakuna mzazi mbaya au mzuri. Ila, malezi ya concerted cultivation yanawapa advantage fulani watoto ukubwani, hasa katika utafutaji wa kazi (job market). Baada ya miaka 15, Lareau alifuatilia maendeleo ya watoto hawa ili kufahamu wanajihusisha na nini. Watoto waliokulia malezi ya concerted cultivation (geti kali) wengi wao wanafanya kazi katika kazi za utaalam (white collar jobs), wakati wengi wa waliolelewa kulingana na modeli ya accomplishment of natural growth walikuwa bado wanabangaiza.

Mara ngapi umemuuliza mtoto swali dogo tu mtaani, na akaficha uso/mdomo na kukujibu kwa kunong'oneza, hii kama hajakupa jibu: "sijui"? Kwanini watoto wengi (hasa wasichana) Tanzania wanakula chakula chumba tofauti na baba mwenye nyumba?

Nchini Tanzania ni aina ya malezi ya accomplishment of natural growth yanayofuatwa na wengi. Hii inachangiwa sana na hali ya umaskini (mfano: mzazi hajui kusoma/kuandika), ila kwa namna kubwa inachangiwa na mila/desturi zetu tulizorithi kutoka mababu. Ni muhimu kutafakari kuwa mila na desturi hizi nyingi hazitatupa advantage yeyote katika dunia ya sasa na kesho ambayo vijana wachakarikaji wanahitajika. Hali ya umasikini wetu kwa namna moja au nyingine inatokana na aina ya malezi tunayokuza watoto wetu.

Jinsi dunia inavyozidi kuwa competitive, ndivyo tunavyotakiwa nasi kubadilika na kujenga taifa la vijana wanaojiamini walio na umahiri wa kuchukua nafasi katika kila anga. Tunahitaji wananchi wasioogopa kuuliza maswali kwa viongozi wao, hivyo wasio rahisi kudanganywa uchaguzi baada ya uchaguzi. Wananchi wa aina hii ndio wasioogopa kuleta mapinduzi katika jamii ili kufuta status quo. Wananchi wa aina hii tutawapata kama tukiwalea watoto wetu kupitia malezi ya concerted cultivation. Ni hivi tu, tutapata wafanyabiashara mahiri, professionals chungu nzima, na muhimu zaidi raia wawajibikaji. We need less submissive citizens and more of whom are ready to take charge.

Nimechoka kusikia kutoka kwa wageni kuwa: “watanzania ni wapole”.

Ningependa kumaliza kwa kumnukuu David Brooks: “todays rich don’t exploit the poor, they outcompete them.”


picha:

http://www.worldvision.org.uk/server.php?show=nav.201

http://imaginationlane.blogspot.com/2010/04/masai-children.html

5 comments:

  1. hehehehe....kuna rafiki yangu alikuwa anasema ukimuangalia hasheem thabeet pia ni mpole. He's as aggresive as other centers in the NBA. Watanzania kweli wapole sisi ndio maana wanyonge.

    Hii pia inaenda hata kwenye elimu. Walimu watakufukuza na kukupa adhabu ukisema "Mwalimu hapo umekosea". Our mentally is to obey and listen to authority (elders,teachers,leaders) without questions.Period.

    I'm BIG, you are SMALL. I'm RIGHT, you are WRONG.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli, mawasiliano darasani kati ya mwanafunzi na mwalimu ni kama hayapo. Mwalimu haulizwi swali.

    ReplyDelete
  3. Bata, huyo rafiki yako hajasikia kisago alichopewa TID? Labda malezi ya Mamtoni yanambadilisha Hasheem..for the better!

    Serious stuff:

    Sasa, mimi nina swali la msingi kidogo -- kabla sijachangia. Upole ni nini? Kwasababu naamini mtu anaweza kuwa mpole lakini akawa ana tabia ya kuuliza maswali na kutaka kujua nini kinachoendelea (bila ya kuwa "mkorofi"); kama mwandishi alivyosema, kwanini natakiwa nifanye hivi. Au "mwalimu/baba, nadhani umekosea hapo."

    Au mwandishi anazungumzia ile hulka ya 'presence'? Kwa mfano, Obama (sio huyu Rais, nazungumzia yule aliyekuwa bado mwanafunzi) nadhani ni mpole, lakini akiingia kwenye kadamnasi ya watu kila mtu atajua jamaa yupo!

    Au nachanganya mambo? Nadhani naliangalia hili suala kwa jicho la tatu.

    ReplyDelete
  4. @anon 2:36.

    Hapa 'Upole' nimejaribu kuuhusisha na dhana ya / desturi ya kuwa 'submissive' kuanzia utotoni na mpaka ukubwani. Wengi wetu hata kama tumelelewa na mila hii ya kuwa submissive, kadili tukuavyo tunapata elimu ya kujua jinsi ya kupigania chetu, na hivyo kujifunza umuhimu wa aggressiveness ukubwani. Ila hii si kwa wote.

    Embu niambie, ukiwa unaongea na mkubwa wako, ni kawaida kumuangalia machoni (eye contact)? Sehemu nyingine mtoto ukimsalimia mkubwa ukimtazama machoni ni kama unavunja protokol. Mimi sikujua umuhimu wa eye contact kwenye mawasiliano ya face-to-face mpaka nilivyoanza kujumuika na watu wa nchi nyingine - hii ni mimi.

    Kama ulivyoeleza, mtu anaweza kuwa mpole lakini akawa anajua yepi ya kusema kwa wakati upi. Na binafsi ninapenda watu wa aina hii. Ila sifa ya 'upole' tulionao watanzania wengi si ya kujivunia. Hali hii inawafanya watu wasiwe na motisha kuuliza maswali kwa wenye mamlaka, MBELE YAO. Mara kwa mara utakuta wanalalamika au wanaeleza vikwazo vyao nyuma ya pazia, majumbani ila wakipewa kipaza cha sauti, kimya! Unless suala liwe linamuathiri yeye binafsi.

    Kumbuka skendo ya EPA. Iligundulika tu, watu makelele meengi. Lakini uliza sasa ni wangapi wanajua matokeo ya kesi hiyo. Unadhani viongozi wangalikuwa wanaogopa kitimoto cha wananchi wangetoa amri ya kuwasamehe wezi wa fedha za EPA pindi wakizirudisha?

    Kwanini watanzania tusijulikane kuwa tu watu aggressive? Aggressive without arrogance that is. Ninaamini kuna underlying factors za kisaikolojia ambazo haziko wazi ambazo zinatufanye tuwe nyuma kimaendeleo kutokana na malezi. Labda mwanasaikolojia anaweza kutupa hint. Achilia mbali historia ya nchi, uchumi wa dunia, n.k

    ReplyDelete
  5. Nimekusoma Joji, na sasa naweza kuchangia :)

    Nilikuwa naogopa kutoa mawazo yangu kwasababu wengine wanahusisha upole na ukarimu na mambo kama hayo. Ambayo nadhani tunapaswa kuyaendeleza kama sehemu ya desturi yetu. Pia, kwasababu waandishi wengi hupenda kurahisisha mambo na ku-generalize. Kwasababu, ulivyosema Watanzania wapole, nikaanza kujiuliza: Mbona watu wanachomwa moto mitaani? Mbona wapokeaji rushwa wanaokandamiza watu wa tabaka la chini bado wanaendelea?

    Nakubaliana na wewe na nisingependa kurudia kwasababu umeelezea vizuri mno! Kwa kuongezea mfano tu, nadhani umekutana na watu ambao kwenye ile mijadala moto moto, wanategemea Watanzania watakubali tu kwa kusema "YES". Na hapo ndipo hatari ya mtu (kutoka nchi nyingine) anadhani amepata mwanya "to walk-over you." Hata kama mtu ana maoni anaamua kunyamaza.

    Binafsi hili suala linanipa hasira kusema ukweli! Juzi juzi nilienda kwenye semina ya kufanya midahala na conflict management. Nilidhani najua mengi... Nikipata muda nitaandika makala hapa Vijana FM.

    Kuna suala jingine ambalo linahusiana na hili ambalo ni ujuzi wa kuwasiliana. Haya matatizo kama yanarandana kwa kiasi fulani. Na nadhani chanzo ni watoto kutokupewa nafasi wakati wanakua (kufundishwa kujieleza n.k.).

    ReplyDelete