Thursday, May 27, 2010

Mlijaribu kuimba kwa ajili ya WOZA 2010?

Na Japhet Joseph

Mashindano makubwa kabisa duniani ya mpira wa miguu - au kama wengine wanavyouita macharange au kabumbu - ndio yananukia; kwa mara ya kwanza kwenye ardhi ya Afrika! Wasanii mbalimabli wamejitokeza kuwashawishi watu wa FIFA kuwateua ili wapate nafasi ya kutumbuiza wakati huo.

K'naan (ft. Bisbal) - Waving Flag:



Shakira - Waka Waka (mlidhani nitausahau huu?):


Lakini baada ya kufaidi mambo kama haya na ukatulia, huna budi kujiuliza: Hivi, mbona sisikii hata wimbo mmoja wa Kiswahili? Wasanii wetu walijaribu kuimba nyimbo kwa ajili ya Kombe la Dunia? Walijaribu kutafuta nafasi ya kutumbuiza? Au DJs wa FIFA/Bondeni wanatubania tu (wanataka mshiko kwanza)?

Kama hamkujaribu, aisee, mmepoteza bonge la nafasi la kuitangaza nchi, lugha na kazi zenu.

Ni mtazamo tu.

2 comments:

  1. Kigezo cha hizi nyimbo sio ngeli? Nisahihishe kama nimekosea

    ReplyDelete
  2. Sijakusoma fresh... Ila ukiacha zile nyimbo 'official', kuna nafasi ya kutumbuiza kwenye sehemu nyingine. Sio kila mtu hupata tiketi na kuishia kuangalia mechi kwenye big screens (kwenye viwanja mbalimbali -- sio lazima vya mpira). Na mara nyingi sehemu hizi huwa na burudani kutoka kwa wasanii kutoka nchi mbalimbali.

    Hata hivyo, kwenye nchi ngapi za Afrika Kiswahili hutumiwa? Ukilinganisha na Kiispanyiola...

    ReplyDelete