Thursday, May 27, 2010

Madenge, Lodi lofa et al

Unakumbuka visa vya akina Komredi Kipepe, Dr. Love Pimbi, Lodi Lofa, Ndumi la kuwili na Madenge kwenye gazeti la SANI ?

Miaka ile, katuni hizi zilikuwa maarufu kiasi kwamba baadhi yetu tulibamkikiwa majina yao kama majina ya utani - nadhani mimi nilikuwa madenge. Mtunzi wa katuni hizi ni marehemu Philip Ndunguru, aliyefariki mwaka 1986 akiwa na umri wa miaka 24. Katuni zake ziliendelea kuleta tabasamu miaka kadhaa iliyofuata. Kwa kumkumbuka mtunzi huyu, na kufurahia kazi zake, embu tazama visa hivi.


10 comments:

 1. Hahahaha! Hii imenikumbusha mbali sana. Shukrani!

  Sasa kwenye masuala ya majina ya utani, mwandishi unadai ulikuwa unaitwa Madenge? Ya kweli haya..Tukamuulize dingi!? Maana'ke kila mtu atajiita MADENGE!

  Mi' nina mdogo wangu, yaani mpaka leo bado tunamuita PEPE (Kipepe). Nadhani inajieleza. Jina langu mimi? Mhhh, nitachuna mpaka wasomaji waseme ya kwao kwanza..LOL.

  ReplyDelete
 2. ...mi walikuwa waniita Pimbi...sasa hata sijui kwanini....

  ReplyDelete
 3. Simpo! Aidha ulikuwa mfupi au ulikuwa ukiona sketi tu unadata! Jibu unalo..LOL

  ReplyDelete
 4. umenikumbusha mbali sana. Asante sana.

  ReplyDelete
 5. hili jarida bado linachapishwa? Mlio bongo nisaidieni.

  ReplyDelete
 6. Enter your comment...dah kitambo sana ila ilikua kiburudisho kizuri.

  ReplyDelete
 7. Sokomoko na Mapung'o walikuwa wachezaji mahiri sana wa soka. Anakupiga katafunua refa anapeta tu mheshimiwa Ndimilakuwili

  ReplyDelete
 8. Sokomoko na Mapung'o walikuwa wachezaji mahiri sana wa soka. Anakupiga katafunua refa anapeta tu mheshimiwa Ndimilakuwili

  ReplyDelete
 9. hello, this is naina from Tanzania. I really like your post and every time I am following your posts. please continue this it's a great job.
  Social Media Marketing Services India

  ReplyDelete
 10. SMARTDIGITALWORK.COM: leading content marketing agency based in Delhi & across India. We can create engaging content to help you promote your website & business on

  Google, Yahoo, Bing etc. At affordable & cheap price. You can search us on Google: content writing services India, content marketing services Delhi, content writing

  services Delhi
  Content Marketing Services Delhi

  ReplyDelete