Samuel Andrew Mbwana a.ka Braton anaelezea nia na madhumuni ya offer hii kwa kusema, “nimeona nitoe offer hii ili mradi wasanii wapate nafasi ya kutosha katika kuelimisha jamii kuhusu uchaguzi wa amani, faida kupiga kura na kuelimisha jamii kuhusu viongozi wanao tufaa katika jamii".
Hii ni changamoto tosha kwa wasanii, hivyo mjitokeze na kuelimisha jamii. Tunatarajia kuona wengi wenu mkijitokeza na kuchangamkia fursa hii ambayo ni adimu. Tukiwa bado tunasononeka na wengi wenu kutojitokeza na kutunga nyimbo kuhusiana na kombe la dunia, basi tunategemea mtatumia hii nafasi vyema kutunga nyimbo kuhusu uchaguzi mkuu.
Habari kwa hisani ya Issa Michuzi
No comments:
Post a Comment