Tuesday, May 11, 2010

Solo Thang arudi na Ung'eng'e!

Juhudi za wasanii wetu kujaribu kuvuka mipaka zinatia moyo na nadhani zimeanza kuzaa matunda. Njia mojawapo ni kutumia lugha ambayo watu wengi nje ya Tanzania wanaielewa. Hii ina faida na hasara zake -- inategemea unaangalia hili suala kwa jicho lipi!

Msanii mwingine ambaye anajulikana na wengi kuwa ana msimamo mkali, Ulamaa amerudi na wimbo mpya unaoitwa 'All I need':Kama ulivyoona, kuanzia mwanzo hadi mwisho ni ung'eng'e tu au lugha ya Malkia, kama mchangiaji mmoja anavyoiita. Binafsi, nadhani jiwe limetulia. Lakini kama mmoja wa washabiki wa Solo Thang, kuna sehemu ya moyo wangu ambayo imetibuliwa.

Solo ana uwezo mkubwa SANA wa kufinyanga na kucheza na maneno ya lugha yetu ya Kiswahili. Kunuka Kunukia, Si Ulinikataa, Sukari na Pilipili, Hili Balaa, Homa ya Dunia...Vina Utata! Natumaini atarudi na nyimbo kama nilizozitaja huku akipiga danadana maneno ya Kiswahili kama Messi.

Hebu jikumbushie njia aliyopitia Msafiri (bofya)! Sikiliza 'Sikati Tamaa', 'Travellaah' na 'Usinichokoze'...

3 comments:

 1. dah!!...steven..yaani huu mpini umewekwa tu kwenye facebook jana usiku mimi baada ya kuusikiliza, nilishikwa na hisia hizo hizo ulizozizungumzia..nikasema nadhani inabidi kampeni yetu ya kumrudisha Hasheem Dogo studio ikamate kasi kama moto mstuni...

  Nyimbo iko poa sana, sema lugha sasa..ikanibidi nimwandikie hichi kipengele solo kama fan wake wa siku nyingi, and it was all out of love

  I see,
  you changed zipcode
  you changed your flow
  we miss the old Solo
  the lyrically untamed
  the Swahili philosopher,
  I know you are
  the traveler, the hustler
  but don’t be blind,
  as you diversify your art,
  coz it was the philosophy
  the Swahili wordplay
  that gave you your crown,
  no crime to explore & grow
  but don’t get sucked in by the ghost
  of pop & commercial thoughts,
  no hate, I’m just looking out
  for Bongo Hip Hop genre,
  it came from far to just die so fast..u know….
  one love Mwanazuoni…..much respect
  & I’ll always be your fan…..am out…

  - this is an extract, I had to, yaani nimetubuliwa imebidi niwa-call out watu wengine fulani fulani..more is to come, this is still in the works..

  ReplyDelete
 2. Natumaini Solo atasikia kilio chetu na kutuelewa. Mzee, umetumia lugha kali...mi' nilikuwa natumia tasfida. Kuna wasanii wengine ambao wanachanganya lugha au kutumia lugha mbili na sijawahi kushtuka kabisa.

  Lakini Ulamaa, kusema ukweli...ni kama Messi yule, badala ya kumuweka mbele apige mabeki chenga na matobo, unamfanya awe golikipa au beki.

  Solo, huu ni mtazamo tu kutoka kwa mashabiki wako.

  ReplyDelete
 3. Nilikua na kiu cha muda mrefu sana kumsikia solo lakini daah..natumaini atatuelewa

  ReplyDelete