Monday, May 24, 2010

Ujumbe kwa TCU & CAS

Tumepata waraka huu kutoka kwa mmoja wa wasomaji wa Vijana FM (Japhet Joseph):

Tanzania Commission for Universities (TUC) ilibadilisha utaratibu wa wanafunzi kujiunga na elimu ya juu kupitia Central Admission System (CAS), ambapo mtu analazimika kutumia simu ya mkononi na mtandao (internet) kuomba nafasi.

Mfumo huu umesaidia kwa kiasi fulani lakini tatizo linakuja kwa wale ambao hawajajiunga mpaka tarehe hizi za mwisho, ambapo mwanafunzi analazimika kukaa kwenye internet café hadi saa tano usiku na kuendelea ili kupata huduma hii -- wakati huu system inakuwa haijaelemewa.

Suala lingine ni kwa wale waliopo vijijini. Hivi wanajua taratibu hizi mpya au wanaendelea kusubiri matangazo ya redio ili wakachukue fomu za vyuo vikuu? Tunaomba wanaohusika na huduma hii waboreshe taratibu hizi nyeti ili wanafunzi wote wapate fursa ya kuomba nafasi kwenye vyuo.

Tunashukuru kwa msaada wenu.

4 comments:

 1. kama nimefanya IB na ninataka kujiunga na UDSM nita'apply vipi?

  ReplyDelete
 2. Miaka mitano iliyopita hiyo kitu ilikuwa haitambuliki. Sijui sasa hivi hali ikoje.

  Labda wahusika wataona ujumbe huu na maswali na kutusaidia. Bahati mbaya inaonekana watoa maoni hapa ni wachache sana.

  ReplyDelete
 3. Wasiliana na Chuo Husika ili kupata mwongozo au unaweza kupata kupia website www.tcu.go.tz
  Kumbuka mwisho ni tarehe 30 Mei 2010 na Pia huduma hii inatumika kwa wale waliomaliza form 6 mwaka 1998 mpaka 2010. Lakini wale wanaotumia sifa linganishi wanachukua form chuoni kama kawaida.

  ReplyDelete
 4. kweli nyabero bora umeona hili naamini ila siombei watu wengi watashindwa kwenda chuo namuombea japhet apate bro huku bongo kila kitu fekiiiiiiiiii MISHETTO

  ReplyDelete