Monday, May 10, 2010

Mic MOJA tu?

Jana nilipata fursa ya kujikumbushia nyimbo za Hasheem. Sizungumzii Hasheem huyu -- namuongelea Dogo! Wakati nasikiliza freestyle inayoenda kwa jina la 'Naharibu' rafiki yangu akanipa wazo la kichokozi... eti tumtafute Dogo, tumuombe arudi ulingoni, tumlipie gharama za studio ili atoea angalau album moja tu.

Tuyaache hayo.

Hivi umeshawahi kujiuliza hili swali: Ingekuwa vipi kama Bongo tungepewa mic moja tu? Yaani, baada ya kuangalia vipaji kadhaa/wasanii mbalimbali, unadhani yupi anastahili kupewa hicho kipaza sauti kimoja tu ili sauti yake iwafakie Vijana wote Tanzania?

Binafsi, napenda wasanii kibao na nawasikiliza wote, lakini kuna mmoja ambaye nadhani atastahili kupewa hiyo mic: N***a Jay, Jay wa Mitulinga, Mti Mkavu, Jay Tunakuzimia, Jay Nyangema, Heavy Weight MC, Prof. Jay...

Tangu Jay atoke na album ile nzito iliyoshiba mawe na vina tokea mwanzo hadi mwisho (Machozi, Jasho na Damu) sidhani kama ametuangusha. Na utakubaliana na mimi kuwa amekuwa kama sauti ya walalahoi.

Wakati muda wa kupiga kura ukikaribia na watu wakiumiza vichwa kura zao ziende kwa nani nadhani labda mambo yangekuwa rahisi mno kama Jay angekuwa mmoja wa wagombea!

Najua wengi mna mawazo tofauti ambayo ningependa kuyasikia. Nani apewe mic?

6 comments:

 1. Kaka, kuna kijana anaitwa Roma. Ana nyimbo tatu tu huyu bwana, lakini anachokiimba humo ndani...mi namfananisha na marehemu Tupac, kwa utetezi wa wanyonge na mashairi yaliyosimama. Bado natafuta nyimbo zake online, na kama nitazipata nitajaribu kuziweka kwa wote wazisikize. Zikoi Tanzania, Mr. President na Nabii (sina hakika na jina, ni nyimbo mpya kabisa). Tanzania inapatikana. Kama bado hujaisikiliza itafute www.dar411.com

  ReplyDelete
 2. Tumpe Roma muda kwanza... najua ana "potensho", baada ya kutoa ALBUMS mbili tatu hivi zenye uzani basi tutaweza kumuweka kwenye sentensi moja na huyo aliyetajwa hapo juu!

  ReplyDelete
 3. Mi nadhani wa kupewa mic moja ni FID-Q

  ReplyDelete
 4. nimemsikiliza Roma..kijana yuko poa..mwanzo mzuri..

  ReplyDelete
 5. Hamko 'siriazz' (no pun intended)..LOL. Mnataka kusema Roma na Fid Q/Mwana FA/Solo Thang wanaweza kugombea Urais na wakaupata?

  ReplyDelete
 6. Mi namuunga mkono Steven..Kusema kweli ukiangalia "consistency", sidhani kama kuna msanii yoyote anamzidi Prof Jay..Jamaa huwa hakosei..Kwa hilo tu, na mimi nampa mic wa Mitulinga..

  ReplyDelete