Friday, March 26, 2010

Tusimsahau Hasheem jamani

Tuliposikia Hasheem kapelekwa D-League Watanzania wengi tulishtuka. Ubaya au uzuri wa tukio hili ni kwamba - kutokana na habari zinavyotapakaa kwenye mtandao kwa kasi - kila mtu alikuwa ana maoni yake, iwe Marekani au Tanzania. Na wengi wetu hatukusita kujadili ingawa hatukujua undani wa suala zima.

Binafsi nadhani alifanya vizuri kwenye kipindi kifupi alichokuwa Dakota Wizards, hasa ukizingatia jinsi kila mtu anayemfahamu au aliyesikia (mambo ya D-League) alikuwa anamtolea mimacho. Inahitaji moyo! Ni wachache sana, hata professionals, ambao wanaweza kufanya alichokifanya; ni mtihani mkubwa sana kisaikolojia. Nakumbuka enzi zile "vidudu" kukariri zile ngonjera za kuwaaga wanafunzi wa darasa la saba ilikuwa 'mbinde'. Lakini baada ya hapo ukiingia darasa la wakubwa mambo huwa mteremko. Kwahiyo ni matumaini yangu kuwa kijana mwenzetu sasa hivi yu tayari kwa vikwazo vingine huko mbele.

Nimekuwa nikiendelea kumfuatilia na bila shaka Hasheem anajitahidi, ukizingatia alipotoka hadi alipo sasa ni safari ndefu sana.


Juzi Grizzlies walifungwa na Golden State Warriors (110 - 128) na Hasheem alijipatia 4 points, 3 rebounds na 3 blocks kwenye dakika 15 alizocheza. Kabla ya hapo alicheza dakika 30 katika mchezo dhidi ya Sacramento Kings ambapo Grizzlies walishinda (102 - 85). Alijipatia 10 points, 7 rebounds na 3 blocks.

Watu mbalimbali kutoka kwenye kikosi cha Grizzlies wamekuwa wakimsifia kwa kuonesha juhudi na maendeleo toka aliporudi kutoka Dakota. Cha muhimu zaidi ni imani ya kocha wake, Lionel Hollins ambayo hasiti kuionesha kila mara watu wa vyombo vya habari wanapomuuliza kuhusu maendeleo ya Hasheem.


Inaonekana vyombo vya habari na blogs zetu zinasahau kutupa habari na fursa ya kujadili au kujifunza mawili matatu pindi mambo yanayotia moyo yanapojiri. Kadri Vijana FM inapokua tutajaribu kumtafuta Hasheem ili atupe picha halisi jinsi anavyojiandaa na mechi za NBA.

Pia napenda kuchukua fursa hii kuwasihi Vijana kuendelea kumpa support Hasheem. Kwa wale ambao ni walevi wa facebook bofyeni hapa.

Nawatakia weekend njema!

2 comments:

  1. Good article on our boy Thabeet. I have watched about 80% of his games (not full games) and he is showing aloot of improvement. He is been playing well since he came back from D-League and since Gasol is injured he has been getting a lot of minutes which I personally believe he has done well enough to get more playing time even when Gasol comes back. Hasheem never said he is the best player out there and if I am correct I think he said "I am a work in progress" like on every interview until i thought he had memorized a monologue for interviews.....I digress ...but the point is he knows he need to work on his game and i am sure he is doing that and article like this when he is doing well or any any positive criticism will help more the negative talk/attacks that he got from a lot of people who didnt know much about what they were talking about.

    ReplyDelete
  2. Kweli, hii mikuno na matawi anayopata kwenye mechi hizi yatamsaidia kujiamini zaidi! Sina uhakika Grizzlies wana nafasi gani kutinga kwenye play-offs; lakini nina uhakika msimu ujao mambo yatakuwa mazuri (Inshaallah, asipoumia tena).

    ReplyDelete