Wednesday, March 17, 2010

Tupeleke macho yetu Mara!

Niliambiwa kuwa fimbo ya mbali haiuwi nyoka! Lakini nakumbuka kuwa niliandika insha kadhaa kubatilisha baadhi ya methali na nahau zetu ambazo kwa namna moja au nyingine haziwezi kutusaidia kwenye baadhi ya mazingira na mazingara.

Najua unaanza kujiuliza maswali kuwa ninajaribu kusema nini haswa leo hii. Usiache kusoma...

Nimeingia 'mzigoni' leo asubuhi mapema, kama kawaida kwa kuanza kuangalia habari kutoka nilipokulia - Tanzania. Bahati mbaya siku imeanza kwa habari zinazosikitisha. Na sisiti kueneza habari zenyewe kama zilivyo; bila ya kuficha chochote kwa kutumia nahau, methali ua maneno mengine matamu.


Mei 24, 2009, Chambi Chachage alitoa taarifa kupitia blog ya Udadisi kuhusu vitendo vya Barrick Gold Mine vya kumwaga takataka za sumu kwenye mto Tighithe, Mara. Athari za takataka hizo kwa afya za watumiaji wa mto Tighithe zilianza kuonekana.

Jana, Machi 16, 2010, Chacha Benedict Wambura wa Foundation HELP alitupa picha halisi ya afya za waathirika kwa kutumia blog ya Udadisi tena. Idadi ya waathirika inazidi kuongezeka na mpaka wakati naandika hii nakala nilikuwa sijapata msamiati sahihi ambao unaweza kuelezea hali ya afya zao.

Kinachotia hasira zaidi ni ukimya wa Serikali yetu na watu wengine husika (uongozi wa Barrick Gold Mine)! Jamani, hawajui haya yanayojiri huko mto Tighithe? Au wamekuwa na roho ngumu kiasi kwamba vitu kama hivi haviwashtui? Hawajali?

Nimeshawahi kusoma visa kama hivi, ambapo urasimu na uchunguzi wa kuhakikisha kuwa takataka kutoka kwenye migodi ndio chanzo cha matatizo kama haya tunayoyaona huchukua miaka. Bahati mbaya wakati muafaka unapatikana vijiji karibu na Tarime vitakuwa vimesha'angamizwa; na hakuna fidia yoyote - kwa watoto na ndugu zao - itakayoweza kuwarudishia maisha yao!

Jamani, viongozi wetu chonde chonde, jamani! Kwenye usahili wa mgodi huu hamkuangalia vitu muhimu kama utupaji wa takataka za sumu? Au, hata hamkutaka kujua ni aina gani ya takataka zitatoka kwenye mgodi huu? Hela mnazopata ndizo zinawafumba macho?

Vijana wenzangu itabidi tufanye chochote tunachoweza kuokoa jahazi - popote tulipo! Fimbo yangu iko mbali, lakini mtandao utanisaidia kumchapa huyu nyoka.


Edit: Ripoti ya Wizara ya Nishati na Madini iliyotolewa Juni 4, 2009 inaishia hivi:

........................................................
Recommendations:
- Local village residents around the mine should be educated on the environmental impacts caused by vandalism and theft of liners...
- There should be timely reporting of various incidents by the mine to the licencing authority.
- It is proposed that liners be covered with compacted thick materials as deterrent to vandalism and theft.
- Mine management should work on ways to ensure that such environmental incidents do not occur in the future.
........................................................

Vipi, mbona suala la afya za waathirika limefumbiwa macho? Watapata fidia za aina yoyote ile?

7 comments:

  1. Hii kitu imenikasirisha sana aise. Sijui nianzie wapi.

    ReplyDelete
  2. well, mpemba nitaanza kwa kusema kikwete 2010..oyeee...jamani rais wetu kijana, tabasamu zuri kweli his the man of the people..

    Nakumbuka zamani kidogo kulikuwa na kesi Marekani ya mji mmoja ulishitaki mgodi fulani, wakashinda na huo mgodi uliwafidia pesa nyingi tu, sasa sijui kisheria Tanzania kama hiyo inawezekana. Mnaweza kuangalia alichofanya Erin Brockovich Marekani.

    Hii ndio inaonyesha na kupima uongozi wa Kikwete, nadhani kutokana na haya serikali inajionyesha yenyewe kuwa ni Serikali ya aina gani. Nasubiri kuona hatua zitakazochukuliwa, sema tushazoea kutoona "actions" zikichukuliwa, hivyo hii inaweza kuwa yale yale tena.

    Nimepata kupitia nakala moja juu ya hiyo Barrick, sema ni ya zamani kidogo..
    http://www.cbc.ca/arts/books/story/2008/05/06/qc-barrickgoldlawsuit0506.html?ref=rss

    ReplyDelete
  3. ukisoma ripoti ya upelelezi ya serikali utaona kuwa walienda kupima pH maji tu. Yaani walitumia litmus paper. dah

    ReplyDelete
  4. Tafiti, hicho ni kitu ambacho siwezi kuelewa kabisa! Nimeisoma ile ripoti nikabaki kutingisha kichwa tu.

    Jana nilipata ripoti za vikao vingine kuhusu sakata hili; inaonekana ni kama wanafanya 'damage control' tu. Nadhani tusipopata majibu ya maana tutaendelea kuchambua hizo ripoti zao kwa kina.

    Cha kusikitisha zaidi ni kwamba inaonekana watu hawajali - kuanzia vyombo vya habari, wahusika wa mgodi, na hata watu wa kawaida ambao wanaweza kusukuma watu kufuatilia nini kinachoendelea Mara.

    Kwa sasa nitamalizia kwa kusema kuna kila aina ya ishara inayoonesha kuwa tatizo kwenye hizo takataka ni kwamba kuna "heavy metals" - Cd, Ni, Pb, Co etc. Angalia link ifuatayo ili kupata mwangaza ya madhara yake:

    http://emedicine.medscape.com/article/814960-overview

    ReplyDelete
  5. Tatizo ni kwamba nchi yetu imetawaliwa sana na ubinafsi,so long as somebody gets something to share with his family,the poor ones always suffer.we seriously need a change in our systems

    ReplyDelete
  6. I've seen that movie on Erin Brockovich. Its simple movie but very touching. It reminds me of the novel Runaway Jury.

    Its very tough fighting against those corporations with influences on every branch of the government. Look at health care in America. It could be done, but its tough. Really tough.

    Most of these cases takes years, it not decades. These guys have money to burn. They hire the best lawyers and fight you to court until you run out of money.

    I'm sure some people have tried speaking out about it. However, someone is doing a darn good job is keeping them quiet. Damage control on point.

    ReplyDelete
  7. Kweli mzee. Ukiambiwa hali halisi na watu wanaofuatilia kinachoendelea ni kama kwenye hiyo filamu.

    Hakika wanajua kuwa kuna watu wanapiga makelele, na wanajua kuwa habari hizi zitatapakaa tu. Sasa je, watu wanaweza kujipanga vizuri na kulivalia njuga hili jambo? Au haliko kwenye damu yetu?

    ReplyDelete