Monday, March 29, 2010

Nabii hakubaliki nyumbani?


Jina: X Plastaz!...Kazi: Hip-hop!...Nyumbani: Arusha!

Unategemea kijana wa kawaida mtaani kutoka Tanzania - ukiacha Arusha - atawajua X Plastaz kwa ufasaha. Lakini, bahati mbaya si hivyo! Ndio, kila mtu ana ladha yake ya muziki na bahati nzuri Bongo imejaliwa kuwa na wanamuziki wa kila aina. Enzi za kuleta wasanii kutoka Kinshasa, Kongo kila Pasaka, au wasanii wa R&B na Hip-hop kutoka 'Unyamwezini' kila Eid zimepitwa na wakati. Leo hii Tanzania ina wasanii wa kila aina wanaoweza kukuna nyoyo za watu.

Na ni kawaida kwa mtu au msanii kuanza kufanya vizuri nyumbani kwanza; kujikusanyia washabiki na heshima, kisha kuanza safari za kujitangaza nje ya nchi. Lakini hii sio njia Vijana wa X Plastaz waliyofuata. Ukiangalia picha zao nyingi wakiwa jukwaani utaona lugha ngeni kwenye mabango, na hii inaonesha 'labda' hawa wenzetu wanaheshimika na kufahamika zaidi nje ya nchi.

Binafsi niliwasikia X Plastaz kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 2000 mwanzoni nilipoenda kusalimia ndugu zangu Arusha. Kaseti (tape) ya album yao ilikuwa imeshiba nyimbo murua kuanzia mwanzo hadi mwisho (ambayo si kawaida kwenye albums za wasanii wengi)!



Bahati mbaya mpaka leo sijapata jibu la kisa cha X Plastaz kutopewa heshima wanayostahili nyumbani. Bila shaka mambo wanayoongelea kwenye nyimbo zao huwagusa wengi, lakini wamewakosea nini DJs wa Dar na Mwanza?

Miaka minne imepita tangu mmoja wao, Faza Nelly alipofariki dunia. Hakika mashabiki wa Faza Nelly na X Plastaz Tanzania na dunia nzima hatutamsahau. Kwa wale ambao hawajawahi kumsikia, sikiliza wimbo ufuatao kwa makini:



Ukitaka kujua zaidi kuhusu hawa Vijana na kuwafuatilia tembelea website yao na ukurasa wao wa facebook. Nadhani ni muda wa X Plastaz kuanza kupewa heshima wanayostahili Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Pia, wale wasanii ambao wana ndoto za kujulikana ughaibuni hawana budi kujifunza kutoka kwao.

5 comments:

  1. Hapa jamaa wana rap hadi kwa kihaya. Hahah, this made my day...
    http://www.youtube.com/watch?v=03uF8AbTU8U

    Uniqueness at its best.

    ReplyDelete
  2. Xplastaz....si mchezo, hawa jamaa kusema ukweli wamepiga hatua. Mimi kila nikizungumzia ubunifu wa katika hip hop, hawa hawagi mbali katika mawazo yangu. Masaai Hip Hop ubunifu, nadhani ndio maana wanatamba ughaibuni, kwani ni tofauti sana na mainstream hip hop. Nchi kama ulaya wanapenda utafauti, lakini Tanzania, tumekumbwa na jini la uroho wa mainstream hip hop.

    Mimi binafsi walivyoanza kusikika nilipenda style yao ya kuchanganya hip hop na umasai, lakini sikuvutiwa saaana na style yao ya kurap. Style yao ilinikumbusha enzi ziile ambapo rap bongo ndo ilikuwa imeanza kushamiri shamiri, enzi za Niggaz2Public, wengi walikuwa wanatumia style ya abigribigri this that this that, kitu ambacho kwa sasa kimepitwa na wakati. Mimi binafsi sipendi sana flow yao, lakini heko zao kwenye ubunifu. Sema nyimbo yao ya mwisho ya Nini Dhambi ilikuwa si mchezo.

    Lakini all in all, inasikitisha kuwa bongo jamaa hawapewi heshima kabisaa, na hata wasanii chipukizi hawataki kujifunza, manake jamaa wamefanikiwa sana kuvuka mipaka milima na bahari, hadi mabara mengine. Nadhani watu wana mengi ya kujifunza kutoka kwao. Tuachane na hip hop katuni.

    Kama hamfahamu, mshiriki mmoja wa Xplastaz alialikwa kwenye BET Awards, kwenye segment ya Cypher. Mcheki GSan akifanya vitu...
    http://www.youtube.com/watch?v=d2wfhGYdMwE&feature=related

    ReplyDelete
  3. Umenikumbusha mbali sana; N2P "Fikiri chini, Vijana kuwa makini" watoto wa Kurasini!

    Najua unapotoka na unapokwenda, Bahati. Unadhani labda ile style yao ndio chanzo cha X Plastaz kutopewa heshima sana nyumbani?

    Ila napenda kutofautiana na wewe kidogo. Ndio walianza na "Ba ba ba ba ba bamizaaaaa", ambayo labda watu waliozoea vinanda vingi kwenye beats za nyimbo za Bongo Flava hawakuipenda sana. Lakini ukiangalia kwa makini utaona kuwa wamekuwa wanabadilika kadri muda unavyoenda kama wasanii wengine waliofanikiwa. Ukisikia nyimbo za "Nigga Jay" enzi zile za 'tongue twist' utanielewa.

    Pata kitu (ft. Fid Q):

    http://www.youtube.com/watch?v=ql4ugeP7e7Y&feature=related

    ReplyDelete
  4. hahah..wewe Steven acha utundu, naona wewe Xplastaz devotee..hahah!!..

    Mimi sidhani style yao ya kughani ndio moja ya sababu, bali nadhani ubunifu wao kwa wabongo wengi ni kitu kigeni (how ironic), ubunifu uliojumuisha vionjo vya nyumbani kwa wabongo vimekuwa so foreign. Sasa ninamaana gani, nina wasiwasi kuwa wabongo wengi tumegubikwa na kasumba kuwa kama hip hop haisound kama ya Marekani basi kuna tatizo. Hatuna ubunifu wa kujaribu kufanya hip hop lakini ikawa yakinyumbani, kama Xplastaz wanavyofanya, congratz nyingi kwao, sema kwa wabongo Hip Hop hapo hapo kimasai, mhhh it doesnt add up..issue ya kasumba. Wewe huoni jinsi hawa akina Beezy na rap zao za Crunk ndio wanakuwa celebrated bongo. Swala ni lile lile, kasumba ya kingereza bongo, kama unaweza kuongea english basi umesoma kweli kweli, ndo hiyo kasumba ikaenda kujikuta kwenye mfumo wa secondary, ambao unasumbua wengi hii issue ya kutumia english kama lugha ya kufundishia.

    Sasa basi, nadhani it comes down to personal preference and choice. Mimi I respect Xplastaz kwa ubunifu wao, lakini inaniwia vigumu kusikiliza style yao ya kughani muda mwingine. Arusha wako na ile mentality ya kuwa na hardcore hip hop kwa sana, kitu ambacho hakiwi celebrated sana, ugumu siku hizi doesnt pay lazima ubalance. Angalia Nako2Nako walikuwa so hardcore, all that gangsta ugumu stuff, but again its style, kama east coast na west coast, styles zinatofautiana kidogo au sio. So ndio kama Arusha na Dar, au kama Temeke na Upanga enzi zile, you can tell utofauti nyimbo Temeke na Upanga.

    Ukipata muda msikilize Witness na nyimbo zake za zamani, neno kufokafoka lilikuwa associated na rap ya bongo enzi zile kwasababu kweli watu walikuwa wanafokafoka zaidi ya kughani. Hiyo siku hizi haipo, unaweza kufoka huku ukighani, lakini ukifokafoka tu, hata utamu wa kusikiliza unakuwa hakuna. Sisemi Xplastaz bongo hawakubaliki kwasababu wanafokafoka na style yao ya ugumu, nadhani style yao ni so unique to the point that its foreign nyumbani. Lakini piga ua, mimi nataka waendelee hivyo hivyo na ubunifu, sema style yao sometimes its hard to listen to na hata kuelewa moja kwa moja nini wanajaribu kusema, na word play yao ya kiswahili huwezi linganisha na akina Jay, Fid Q etc etc...

    All in all, much respect kwa Xplastaz hao jamaa ni wabunifu, the only problem I personally have with them ni style yao ya kurap sometimes is just not that interesting.

    Hao jamaa wangetafutwa nao watoe maoni yao, mbona hawakubaliki nyumbani?..au kuna mkono wa mtu..hahah..manake majuzi Q Chief alilalamika kurogwa na T.I.D ndio maana mambo yake yamekuwa yakienda mrama kwa muda sasa..hahah!!

    ReplyDelete
  5. Nimekuelewa mzee. Nina maoni mengine lakini nadhani niko 'biased', kwasababu napenda kusikiliza mtu anayenifanya nifikirie.

    Kuhusu style, kuna wale madogo wa Manzese Crew waliokuja na "Kula kona". Kuna vitu kadhaa ambavyo vinafanana na X Plastaz (Ba ba ba ba ba ba bamizaaaa), lakini nyimbo yao ilikuwa inachezwa sana kuliko nyimbo yoyote ile ya X Plastaz.

    Pia, ni ngumu sana kwa mtu kutoka Unga Limited (Arusha huko uswazi..kama TMK fulani) aimbe mambo ambayo sio ya 'kigumu'.

    Nitafanya juhudi zangu kumtafuta G San aje ulingoni atupe maoni yake.

    LOL @ Q Chief kupigwa ndumba...Uswazi wanasema kapigwa kipapai.

    ReplyDelete