Monday, April 12, 2010

Matumizi ya 'sms' katika mapambano dhidi ya Ukimwi




Nchini Afrika Kusini mapambano ya kupunguza vifo kutokana na Ukimwi yameingia sura mpya. Wenzetu wameanza kutumia huduma ya simu za mkononi katika mapambano hayo. Inafahamika kuwa Afrika ni sehemu yenye waathirika wengi wa ugonjwa huu duniani. Bara hili pia lina idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi (zaidi ya milioni 300). Mwaka 2008 shirika la Praekelt kupitia mradi wa Masiluleke walianzisha huduma iitwayo TxtAlert yenye nia ya kuwakumbusha ahadi za hospitalini/zahanati waathirika wa HIV walio katika matibabu.

image: http://www.poptech.org/project_m

Nchini Tanzania kuna huduma ya ujumbe fupi utumwao bure ujulikanao kama „tafadhali nipigie“, huduma bure ya TxtAlert ya wenzetu huko bondeni ni kama hii ila ujumbe utumwao unaenda kwa hospitali/zahanati na wao kwa kushirikiana na mshirika wa TxtAlert wanakukumbusha appointment yako. Kwa kutumia huduma hii, waliosajiliwa wanaweza pia kubadili ratiba ya appointment kama waliikosa.

Wenzetu wanachotaka kupunguza ni ukithiri wa waathirika wasioenda hospitalini kupokea dawa, tabia ambayo inaweza sababisha ‘ukuaji’ wa virusi vya ukimwi (HIV) sugu. Huduma hii pia inawasaidia wauguzi kupunguza msongamano ulio holela unaotokea baada ya watu kusahau au kukosa appointment zao. Mradi huu unaendelea nchini Afrika ya Kusini na mpaka sasa zaidi ya watu 10000 wamesajiliwa, na manufaa kadhaa yameonekana. Ingependeza pia kusikia nchini Tanzania makampuni ya simu au taasisi za teknolojia wakizindua huduma hii kwa kushirikiana na zahanati zinazotoa HIV therapy.


muasisi wa mradi wa Masikulele, Gustav Praekelt akitoa mada katika kongamano la Poptech 2008 (picha na Kris Krüg)

No comments:

Post a Comment