tag:blogger.com,1999:blog-2653305789535496384.post6499238746183930773..comments2024-02-19T00:19:54.560-08:00Comments on Vijana FM: Penye Kufuka MoshiVijana FM (admin)http://www.blogger.com/profile/03776012696907867956noreply@blogger.comBlogger1125tag:blogger.com,1999:blog-2653305789535496384.post-54912254643180906882010-05-10T06:16:04.583-07:002010-05-10T06:16:04.583-07:00Umegusia kila kona; nitajaribu kukupa mawazo yangu...Umegusia kila kona; nitajaribu kukupa mawazo yangu kwa kifupi (kwanza).

1. Tatizo au chimbuko la haya matatizo ni watu kwenye bongo flava (wasanii na DJs) kujifikiria wenyewe na kutokuona mbali. Hawaoni jinsi muziki kwa ujumla unavyoweza kubadilisha maisha ya vijana wengi. Hawaoni MNYORORO unaowaunganisha kuanzia kwa producer mpaka yule dogo anayesukuma kitoroli au kuendesha kaguta cha kaseti. Kwahiyo, kama unahusika na bongo flava, fungua macho na wafikirie wengine. Nadhani huo utakuwa ni mwanzo wa kuanza kuijali na kuitetea bongo flava kama mboni za macho yetu!

2. Hivi wasanii na hao DJs wameshaanza kufikiria watafanya nini baada ya "kustahafu"? Namaanisha...wasanii na DJs hawawezi kuendelea kufanya wanachofanya sasa hivi. Kwahiyo, ni muhimu kuitunza na kuhakikisha bongo flava inaendelea ili hapo baadae uwe kama 'mtaalamu' kwenye nyanja fulani (iwe kuandika vitabu kuhusu historia ya bongo flava, misukosuko iliyokupata wakati uko kijana n.k.). Lakini kama bongo flava ikizorota, unadhani kama msanii utakuwa na cha maana cha kufanya???

3. Wasikilizaji sio wajinga. Ipo siku watu wataamka tu. Utapiga nyimbo za mtu fulani kila siku; halafu ukienda kwenye show utakuwa peke yako na msanii wako "mpendwa". Chema chajiuza, kibaya chajitembeza...

4. Muungano na umoja. Mpaka sasa hivi siamini wasanii bado wanawategemea mapromota. Hawawezi kujiunga na kuunda kama kampuni hivi ya kuwasaidia kuandaa shows? Au usambazaji wa kazi zao? Kila msanii hawezi kuchangia 50,000 ili kuanzisha kampuni kama hii?

5. Chipukizi v. Wakongwe. Hiyo ni kawaida na halinipi wasiwasi; lakini kuna wale wakongwe ambao hubadilika kadri muda unavyoenda na tunajua wataendelea kufanya vizuri. Mifano tunayo (angalia post hapo chini).

Kwa kifupi, itabidi Vijana tujifunze kuangalia na kuona mbali. Leo mkono unaenda kinywani, kesho je? Utunzeni huu muziki na sanaa kwa ujumla kama misahafu.SNhttps://www.blogger.com/profile/09052751960069005719noreply@blogger.com